Aidha, Serengeti imenyakua nafasi ya tatu Nyuma ya Mauritius and Kathmandu kwenye kitengo cha Maeneo Bora ya Asili - Ulimwenguni.
Serengeti imeyapiku maeneo mengine Barani yakiwemo mbuga za wanyama, na sehemu za pwani huku ikipigiwa kura kwa kura sehemu yenye huduma dora za kitalii na mvuto zaidi.
Hii ni baada ya kupigiwa kura na watalii kupitia tovuti ya Tripadvisor, unaotumika na zaidi ya watalii na wasafiri milioni 400 kote ulimwenguni.
Mbuga ya kitaifa ya Tanzania ya Tarangire imechanguliwa kuwa eneo la saba Afrika lenye kivutio cha juu huku ikimaliza kwenye nafasi ya saba katika kitengo cha maeneo yenye vivutio bora zaidi.
Mbuga hiyo pia ina umaarufu wa kuwa na idadi kubwa zaidi ya tembo nchini Tanzania mbali na kuwa na wanyama pori wengine.
Kuhusu Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, hifadhi hiyo inafahamika kwa kidimbwi cha Viboko Serengeti, Seronera, Mto Mara, na Mto Grumeti.
Wamasai huita tambarare za Hifadhi ya Kitaifa ya Serengeti "mahali ambapo ardhi huendelea kusonga mbele milele"
Serengeti imetambulika na kupata sifa kwa uhamiaji maarufu wa kila mwaka wa Serengeti, ambao ndio uhamiaji mkubwa na mrefu zaidi wa ardhini duniani.
Kisiwa cha Nungwe kilichaguliwa kuwa fukwe bora zaidi Afrika kwenye kitengo cha fukwe bora Barani Afrika.