Wamasai wa kutoka Ngorongoro waghadhabishwa na hatua ya Serikali ya Tanzani kuwahimisha kutoka ardhi yao ya asili. /Picha: Wengine

Na Mustafa Abdulkadir

TRT Afrika, Istanbul, Uturuki

Chama cha CHADEMA siku ya Jumanne, 20 Agosti kilitoa taarifa kupinga wananchi wa Tarafa ya Ngorongoro kuondolewa kwenye ardhi yao.

Taarifa hio inasema,“Tunapinga amri ya Serikali iliyochapishwa kwenye Gazeti la Serkali namba 673 la tarehe 02 Agosti, 2024. Amri hio imewaondoa wananachi wote wa Tarafa ya Ngorongoro kwenye ardhi yao kwa kufuta Kata, Vijiji, na Vitongoji vyote vya Tarafa hiyo.”

Vilevile kwenye taarifa hio, chama cha CHADEMA kimelaani kitendo cha serikali kusitisha huduma za kijamii kwa wananchi hao kama vile huduma za afya, elimu na pia kusitisha miradi yote ya maendelo.

Aidha chama hicho pia kilikemea hatua ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kutaka waheshimu Katiba ibara ya 74 na Sheria ya Tume ya Uchaguzi na hivyo kurejesha majina ya wapiga kura kwenye daftari la kudumu la wapiga kura walipojiandikisha kisheria.

Mwisho kabisa Chama hicho kimetoa wito wa kwa serikali kufanya mazungumzo na wananchi hao na kufutulia mbali amri hiyo, wakisema kutobatilishwa amri hiyo kutasababisha maafa makubwa kwa wananchi na Ngorongoro na kuhatarisha amani ya nchi.

Wananchi hao wa Ngorongoro wa kabila la Masai wana uwezekano wa kukosa ardhi na makazi yao na kuhamsihwa hadi eneo la Msomera Tanga, kwa sababu ya upanuzi wa Hifadhi wa Ngorongoro.

TRT Afrika