Siobhan Brady anafanya kampeni dhidi ya ugonjwa wa ' cystic fibrosis' / Picha: Highest Harp Concert

Mpiga kinubi kutoka Ireland ameweka rekodi mpya ya tamasha la juu zaidi la wapiga vinubi wakati wa onyesho la dakika ishirini katika Mlima Kilimanjaro nchini Tanzania - kilele cha juu kabisa barani Afrika .

Alifanya tamasha hii kama kampeni ya kusaidia wale wanaoishi na ugonjwa wa cystic fibrosis.

Cystic fibrosis ni ugonjwa wa kurithi ambao huunda kamasi nene ambazo hunata nata hasa kwenye mapafu na kongosho.

Onyesho lililojumuisha utunzi wa kitamaduni na wa kisasa/ Picha: Highest Harp Concert

Siobhan Brady mwenye miaka 24, alipata mafanikio hayo Jumanne katika onyesho lililojumuisha utunzi wa kitamaduni na wa kisasa kutoka Ireland, na pia ulijumuisha uimbaji wa wimbo wa " little bird" wa muimbaji kutoka uingereza, Ed Sheeran.

Brady ndiye anayeshikilia rekodi ya sasa ambayo aliweka mnamo 2018 katika safu ya milima ya Himalaya.

Brady alifanya tamasha wa usaidia wa Waafrika /Picha: Highest Harp Concert

Aliwasili Tanzania wiki iliyopita na timu yake ya wachezaji 19 kufuatia miaka ya mipango na mafunzo nchini Ireland, kulingana na taarifa kwa shirika la Highest Harp Concert.

"Imekuwa tukio lisiloweza kusahaulika, lenye thamani na changamoto kwa kiwango sawa na najua ninazungumzia kutoka timu yote ninapomshukuru kila mtu ambaye alituma ujumbe kutoka mbali," alisema.

Onyesho la Brady lilijumuisha wimbo ya Kitanzania inayomaanisha ‘Asante Tanzania’ kwa Kiswahili. Msemaji wa serikali ya Tanzania Gerson Msigwa ni miongoni mwa waliompongeza Brady kwa mafanikio yake.

Mafanikio hayo yalifikiwa kwa usaidizi wa timu wa Waafrika takriban 60.

Rekodi hiyo mpya haijathibitishwa na shirika la rekodi za dunia la Guinness Book of World Records.

TRT Afrika