serikali ilikuwa imetangaza Agosti 22 kuwa inapanga kuandaa kura ya maoni kubainisha hali ya eneo linalozozaniwa na mikoa ya Tigray na Amhara/ Picha : Reuters

Takriban watu 183 wameuawa katika mapigano tangu mwezi Julai, kulingana na taarifa zilizokusanywa na afisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa.

Hii ni kufuatia mapigano yaliyoisha kati ya jeshi la Ethiopia na wanamgambo wa kikanda wa Fano, na kutangazwa kwa hali ya hatari mnamo Agosti 4, hali ilizidi kuwa mbaya zaidi.

Umoja wa Mataifa umeelezea kufadhaishwa na hali ya hatari iliyotangazwa nchini humo ambayo wanadai inapatia serikali nguvu kubwa kuwakamata washukiwa na kuweka marufuku ya kutoka nje pamoja na kufanya mikutano.

''Tumepokea ripoti kwamba zaidi ya watu 1,000 wamekamatwa kote Ethiopia chini ya sheria hii,'' imesema ripoti hiyo.

''Wengi wa waliozuiliwa waliripotiwa kuwa vijana wa kabila la Amhara wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa Fano.'' iliendelea kusema.

Serikali haijatoa majibu yoyote kuhusiana na ripoti hiyo.

Hata hivyo awali serikali ilikuwa imetangaza Agosti 22 kuwa inapanga kuandaa kura ya maoni kubainisha hali ya eneo linalozozaniwa na mikoa ya Tigray na Amhara nchini humo.

Waziri wa ulinzi wa Ethiopia Abraham Belay alinukuliwa kusema kuwa, ''Serikali imeapa kufuta kile ilichokiita "utawala haramu" katika eneo linalosimamiwa na Amharas, huku ikitafuta mbinu zote za kuleta suluhu kwa njia ya amani.''

TRT Afrika