Ethiopia inapakana na Sudan katika eneo lake la Amhara  / Picha: Reuters

Mamlaka ya jimbo la mashariki la Al-Qadarif nchini Sudan yafunga mpaka wake wa Gallabat na Ethiopia siku ya Jumapili baada ya wanamgambo wa Fano kutoka Ethiopia kuuteka mji wa karibu wa Ethiopia wa Metemma.

Hii ni kulingana na vyombo vya habari nchini Sudan.

Mkoa wa Amhara nchini Ethiopia ambao unapakana na Gederaf, umekuwa na mapigano ya mara kwa mara kati ya Fano na vikosi vya serikali tangu serikali ya Ethiopia kutia saini makubaliano ya amani na vikosi vya Tigray mnamo 2020.

Vyanzo vya habari nchini humo vilisema mamlaka ya Sudan iliruhusu polisi wa shirikisho la Ethiopia na wanajeshi kuvuka hadi Sudan baada ya kusalimisha silaha zao.

Kwa upande wake, kikundi cha Fano kiliwaruhusu Wasudan waliokwama mpakani kuvuka kuingia Ethiopia.

Maelfu ya raia wa Sudan wamevuka hadi Ethiopia kupitia Gallabat tangu mzozo ulipozuka nchini Sudan mwezi Aprili 2023 kati ya jeshi na kikosi cha kijeshi cha 'Rapid Support Forces' (RSF).

Fano inaripotiwa kuteka mpaka wa huko Metemma, ikidaiwa kulenga kuzuia usambazaji wa mafuta na chakula kutoka Sudan kuingizwa mkoa wa Amhara.

TRT Afrika