Na Charles Mgbolu
Mashabiki wanampongeza mtayarishaji wa muziki wa Ghana Kwabena Ofei-Kwadey Nkrumah baada ya kushinda kesi ya haki miliki dhidi ya Shirikisho la Soka Afrika.
Kwabena, anayejulikana katika ulingo wa muziki kama Spiky, alifidiwa $250,000 na Mahakama ya Biashara 7 mjini Accra baada ya kuishitaki CAF mwaka wa 2019 kwa kutumia sehemu za wimbo wake wa 'Okomfo Anokye' katika kipindi cha utangazaji wa Tuzo za CAF za 2018.
CAF haijajibu matukio ya hivi punde, lakini sehemu ya 'Sheria na Masharti' kwenye tovuti yake yanasema "inaheshimu haki miliki ya wengine."
Spiky aliviambia vyombo vya habari vya ndani baada ya ushindi huo muhimu Jumatano, kwamba aliiandikia CAF mara nyingi na kutuma ujumbe kwenye mitandao ya kijamii akiomba sehemu za wimbo wake kuondolewa, na kufuatiwa na fidia mwanzo, bila mafanikio.
Spiky alisema video za matangazo zilikaa mtandaoni hadi baada ya tuzo za CAF 2018, ambazo zilifanyika Januari 2019.
Video hiyo yenye utata picha za wasanii walioteuliwa kuwania Tuzo za Mchezaji Bora wa Mwaka wa CAF 2018 (kategoria za wanaume na wanawake). Iliwekwa mtandaoni kama nyongeza ya sherehe ya tuzo, ambayo ilifanyika Dakar, Senegal.
Video hiyo ilikuwa na midundo ya Kiafrika ikicheza muziki ambao Spiky alidai kuwa ulitoka katika kazi yake ya muziki wa 'Okomfo Anokye'.
Kipengele cha sita katika Sheria na Masharti ya CAF inasema: "Ikiwa unaamini kuwa haki zote za historia zimekiukwa kwenye Mifumo ya Dijiti ya CAF, tafadhali ipe CAF habari ifuatayo: majina yako kamili, anwani, barua pepe, aina ya ukiukaji, na kiwango cha ukiukaji (tarehe, wakati, n.k.).
'Ushindi kwa wabunifu wote'
Licha ya kufuata miongozo hii, Spiky anasema aliamua kufika kortini baada ya kutopata jibu kutoka kwa CAF kuhusu suluhu hiyo.
Siku ya Jumatano, Spiky aliambia vyombo vya habari vya nchini Ghana Citinewsroom, “Ushindi huu si wa kwangu tu; ni ushindi, haswa kwa wabunifu wote na kwa vijana wa Ghana ambao wamepoteza imani.
"Spiky pia ali "retweet" ujumbe wa pongezi kutoka kwa mwanablogu Mghana wa mtandaoni na mwanablogu wa teknolojia aliyeshinda tuzo MacJordan, ambaye aliandika, "Kudos, @therealSpiky, kwa kupigana na hili hadi mwisho.
Hii ni kielelezo kwa wabunifu wote wa Kiafrika kutetea haki miliki zao."
Okomfo Anokye, wimbo wa sauti wa dakika 3 na sekunde 15, ulitolewa mnamo Juni 20, 2015, kwenye tovuti ya utiririshaji wa Soundcloud.