Rais mstaafu Jakaya Kikwete ametumikia taifa katika nyadhifa mbali mbali pamoja na nafasi za kimataifa kabla na hata baada ya urais. / Picha : Ikulu Tanzania 

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaongoza viongozi wengine pamoja na wananchi wa Tanzania kumminia pongezi rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwa maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa,

''Heri ya miaka 73 ya kuzaliwa Mheshimiwa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete.'' Alise,ma mama Samia katik aukurasa wake wa X, zamani Twitter. ''Ahsante kwa utumishi wako kwa umma wa zaidi ya miaka 50 kwenye Chama Cha Mapinduzi, Jeshi la Wananchi wa Tanzania, na baadaye kama Rais wa nchi yetu. Nakutakia afya njema na wakati mwema unapokumbuka siku hii,'' aliongeza.

Mheshimiwa Rais Kikwete, alizaliwa mjini Msoga, Tanzania tarehe saba Oktoba mwaka wa 1950.

Jakaya Mrisho Kikwete ni mwanasiasa wa Tanzania ambaye alikuwa rais wa nne wa Tanzania, madarakani kuanzia 2005 hadi 2015.

Kabla ya kuchaguliwa kuwa rais, alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje kuanzia 1995 hadi 2005 chini ya mtangulizi wake, Benjamin Mkapa.

Rais Kikwete ana Shahada ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na sasa ni Mkuu wa Chuo hicho. Pia ni Luteni Kanali mstaafu katika jeshi la Tanzania.

Katika maisha yake yote ya utumishi wa umma, katika serikali ya Tanzania na baadaye katika mashirika ya kimataifa na kikanda, Rais Kikwete amejitolea kuendeleza sera za maendeleo za elimu na afya ya wanawake na watoto

Baada ya kustaafu serikali, Rais Kikwete aliwahi kuwa mjumbe maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Kufadhili Fursa ya Elimu Duniani, akiongoza wajumbe wa ngazi za juu katika nchi 14 barani Afrika.

TRT Afrika