Nyerere anaendelea kusifika sio Tanzania Pekee bali Afrika na dunia nzima kwa mtazamo wake wa utangamano na umoja,/ Picha : Ikulu 

Oktoba 14, inakumbukwa na Watanzania kama siku ya kumsherehekea mwanzilishi wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Wananchi wa tabaka mbali mbali walikusanyika katika maadhimisho hayo ya miaka 24 tangu kufariki Rais Nyerere.

Rais Samia Suluhu Hassan alikuwa miongoni mwa waumini waliokusanyika katika kanisa katoliki la Parokia ya Roho Mtakatifu, Babati Mkoani Manyara

''Tumetimiza miaka 24 tangu kuondokewa na kiongozi huyu mahiri, mmoja ya waasisi wa Taifa letu,'' alisema Rais Samia baada ya misa hiyo. ''Tunajivunia misingi aliyotujengea, inayoendelea kutufanya kubaki Taifa moja, lenye amani na mshikamano. Misingi ambayo kila mmoja katika nchi yetu analo jukumu la kuendelea kuitunza, kuilinda na kuisimamia,'' aliongezea Rais.

Rais Samia Suluhu alijiunga na wumini kwa sala maalum ya kumuombea marehemu Julius Nyerere./ Picha : Ikulu Tanzania 

Shughuli za maadhimisho haya zilianza tangu mapema asubuhi ambapo Rais Samia Suluhu alijiunga na wumini kwa sala maalum ya kumuombea marehemu Julius Nyerere.

Sifa zisizo na kifani

Julius Kambarage Nyerere, aliyeitwa pia 'Mwalimu' , alizaliwa Machi 1922, kijijini Butiama, na alikufa Oktoba 14, 1999, mjini London, Uingereza. Alikuwa waziri mkuu wa kwanza wa Jamhuri ya Tanzania.

Nyerere anaendelea kusifika sio Tanzania Pekee bali Afrika na dunia nzima kwa mtazamo wake wa utangamano na umoja, hasa alipopigania sana kuungana kwa Afrika katika maendeleo.

Pia Marehemu Rais Nyerere alikuwa mstari wa mbele kutafuta umoja wa Afrika katika masuala mengi, ikiwemo kuikuza lugha ya Kiswahili kama lugha ya Afrika, itakayotumiwa kama chombo cha kuwaunganisha watu.

Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Mwenge kutoka kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Abdallah Shaibu Kaimu wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha mbio hizo/ Picha : Ikulu Tanzania

Nchini Tanzania, ameendelea kusifika kama kuinganishi wa taifa. Hadi sasa vizazi vyote vinamtambua na kumpa heshima ya juu zaidi na wengi wanafuata itikadi yake ya Ujamaa, umoja na ushikamano miongoni mwa Watanzania.

Katika maadhimisho ya Kumbukizi ya Nyerere, mwenge wa taifa ulizungushwa ambapo kilele ilikuwa hafla ya kumpokeza Rais Samia Suluhu Hassan mwenge huo katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati Mkoani Manyara.

TRT Afrika