Inaripotiwa kuwa mkuu wa Shirika la IMF Kristalina Georgieva alifanya mazungumzo na Rais William Ruto baada ya kukataa kwake  kusaini Muswada wa fedha 2024. / Picha Wengine

Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, lilisema siku ya Alhamisi kwamba linatathmini matukio ya hivi majuzi nchini Kenya. Imeongezea kuwa programu zake za utahmini ni fursa ya kurekebisha changamoto kufuatia maandamano mabaya ambayo yalikuwa sababu ya serikali ya kutotia saini muswada wa fedha 2024.

Mapendekezo ya muswada huo ungechangia dola bilioni 2.7 katika nyongeza ya ushuru.

"Katika kila mapitio ya programu tunachukua fursa ya kutathmini na kufanya marekebisho kwa kuzingatia mazingira mahususi, na hivyo ndivyo tunavyofanya katika majadiliano yetu ya kina na mamlaka ya Kenya," msemaji wa hazina Julie Kozack alisema katika vyombo vya habari.

Timu ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), ikiongozwa na Haimanot Teferra, ilifanya majadiliano na mamlaka ya Kenya mjini Nairobi, mnamo Aprili 2-12 na Mei 9-15, 2024.

Ujumbe uliendelea kwa makini kukamilisha vipengele muhimu vya kiufundi vya makubaliano hayo, ikiwa ni pamoja na kurekebisha upya upatikanaji wa rasilimali za IMF ili kuwianisha kwa karibu zaidi na mahitaji ya sasa ya Kenya.

" Upungufu mkubwa katika ukusanyaji wa mapato ya kodi, na kuzorota kwa salio la msingi la fedha katika Mwaka wa Fedha wa 2023/24 ikilinganishwa na malengo ya programu inatarajiwa kuweka mahitaji ya ukopaji wa ndani kuwa juu," ameongezea.

"Kwa sababu hiyo, malipo ya riba yameongezeka, na hivyo kuweka shinikizo kwa deni la umma hata baada ya deni hilo kunufaika na kuimarishwa kwa shilingi ya Kenya."

Mpango wa IMF ulitarajiwa kutoa Ksh124 bilioni (dola milioni 976) katika ufadhili wa nje, katika mwaka wa fedha wa 2025 au karibu theluthi moja ya ufadhili wa nje uliopangwa na serikali.

Kauli ya IMF inajiri wiki moja baada ya Rais William Ruto kufanya mazungumzo kwa njia ya simu na mkuu wa Hazina hiyo, Kristalina Georgieva ambapo wawili hao walijadili masuala kadhaa kuhusu kuondolewa kwa mswada wa fedha uliopigwa na chini na rais huyo.

Muswada wa fedha 2024 ambao rais William Ruto amekataa kutia saini, ulijumuisha mabadiliko ya msingi ya sera yaliyokubaliwa na Kenya na IMF kama sehemu ya mpango wa mikopo wenye thamani ya dola bilioni 3.6.

TRT Afrika