Serikali ya Kenya yaelekeza kidole cha lawama kwa 'waandamanaji wa fujo'

Serikali ya Kenya yaelekeza kidole cha lawama kwa 'waandamanaji wa fujo'

Waziri wa usalama wa ndani amekanusha kuwa jeshi la polisi lilihusika katika 'mauaji ya waandamanaji'
Minister for interior Kenya

Waziri wa Kenya wa usalama wa ndani Kithure Kindiki ametoa onyo kali kwa wote waliohusika katika maandamano yaliyoisjia kwa ghasia katika miji mikuu nchini humo, kuwa watakabiliw anamkono wa sheria.

Waziri Kindiki pia amekanusha madai ya baadhi ya viongozi wa upinzani kuwa jeshi la polisi lilihusika katika mauaji, huku akielekezea kidole cha lawama kwa waandaaji wa maamndamano hayo aliyoyataja kuwa yalilenga kuvuruga amani na uendeshaji wa serikali.

''Madai kuwa maafisa wa Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) na watekelezaji sheria wengine wanahusika katika mauaji au utumizi mbaya wa mamlaka dhidi ya umma ni uongo na iliyokusudiwa kupotosha maoni ya umma kuhusu uhalifu wa hivi majuzi ambao ilifanyika katika baadhi ya maeneo ya nchi.'' Waziri Kithure amesema katika taarifa kwa vyombo vya habari.

POlisi wamethibitisha kuwa watu 7 walifariki wakati wa maandamano hayo yaliyoishia kwa ghasia : PIcha 

Kurushiana lawama

Upinzani umetoa lawama kuwa zaidi ya watu 50 waliuawa na polisi wakati wa maandamano wanayodai yalikuwa ya amani kulalamikia gharama ya maisha. Serikali imesisitiza kuwa idadi hiyo ni 7 pekee.

Kiongozi wa muungano wa upinzani (Azimio) Raila Odinga, ameshutumu polisi kutumia nguvu kupita kiasi katika kutawanya waandamanaji hao.

''Watunzi wa habari hizi za uongo na potofu ndio wa kulaumiwa zaidi kwa kupanga, kufadhili na kutekeleza uhalifu wa kutisha uliosababisha vifo na majeraha ya raia na maafisa wa polisi pamoja na uharibifu wa mali ya kibinafsi na ya umma katika wiki chache zilizopita.'' Taarifa hiyo imeongeza kusema.

Raila Odinga, ametangaza Jumatatu kuwa amefuta maandamano yaliyoitishwa kufanyika Jumatano akisema badala yake watakwenda kuomboleza pamoja na jamaa za waliouawa katika maandamano.

Kenya Protests

Makadirio ya hasara

Wakati huo huo, waziri Kindiki amesema kuwa serikali imeshutshwa na uharibifu uliosababishwa na wanadamanaji waliowataja kuwa wahuni.

''Baada ya kutathmini matokeo ya ghasia hizo, tunathibitisha kwamba nchi imebakia kuhesabu hasara kubwa ambayo ingeweza kuepukika,'' imeendelea kusema taarifa.

Kwa mujibu wa waziri Kithure KIndiki hara iliyopatikana ni:

  • Maafisa 305 wa polisi wamejeruhiwa vibaya.

  • Afisa mmoja wa polisi aliuawa alipovamiwa na waandamanaji.

  • Magari 158 za polisi yamechomwa.

  • Vituo 9 vya polisi vimeteketezwa.

  • Zaidi ya maduka 850 yamevunjwa na kuporwa mali ya thamani isiyojulikana

  • Majumba 199 zimeharibiwa na mali ya umma ya thamani ya mabilioni kuharibiwa.

  • Kesi 156 za uhalifu na uvamizi zimewasilishwa katika vituo vya polisi

Waziri Kithure ameongeza kuwa, uchunguzi utakapomalizika, wote waliohusika katika ghasia hizi watapata adhabu kamili kisheria.

TRT Afrika