Kama ilivyo kawaida, nchi za Afrika ziliongoza kwa kupokea wageni wengi zaidi waliotembelea vivutio mbalimbali barani humo./Picha: AFP 

Na

Mwandishi Wetu

Sekta ya utalii barani Afrika imeanza kurudi katika hali yake ya kawaida baada ya janga la Uviko 19, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.

Takwimu hizo zinaonesha ongezeko la asilimia saba katika idadi ya watalii kwa mwaka 2024, ukilinganisha na 2019, mwaka mmoja kabla kutolewa zuio la kusafiri.

Afrika ilipokea asilimia 12 ya wageni zaidi kwa mwaka 2024 kuliko mwaka 2023, imesema takwimu hiyo.

Upande wa Kaskazini wa Bara la Afrika ndio ulioshuhudia idadi kubwa sawa na asilimia 22 kwa mwaka 2024.

Jumla ya watalii bilioni 1.4 walitembelea maeneo mbalimbali ulimwenguni kwa mwaka 2024.

Kama ilivyo kawaida, nchi za Afrika ziliongoza kwa kupokea wageni wengi zaidi waliotembelea vivutio mbalimbali barani humo.

Kwa mfano, nchi ya Morocco ilipokea watalii milioni 14 kwa mwaka 2023.

Nchi hiyo imejiwekea lengo la kupokea watalii milioni 17.5 ifikapo mwaka 2026 kupitia kuanzishwa kwa safari mpya za ndege.

Wakati huo huo, mapato ya utalii nchini Kenya yalikua kwa kasi kufuatia kuwasili kwa watalii milioni 19.5, huku ikiwa imejiwekea malengo ya kupokea watalii milioni 2.4 mwaka 2024.

TRT Afrika