Na Mengesha Michael
Hapo awali Afrika ilijulikana kama "Bara la Giza" na mwandishi wa habari wa Wales na mgunduzi Henry Morton Stanley, ambaye aliona Afrika kuwa ya ajabu.
Watu wengi kutoka nje hawakuwa na ufahamu wowote wa tamaduni na mandhari ya ardhi yake, mpaka ilipofikia karne ya 19.
Mara kwa mara, historia ya Afrika hufunikwa na simulizi za vita, shida, na mapambano ambayo huendana na simulizi zisizotajwa.
Hata hivyo, bara hilo linashikilia rekodi kongwe zaidi duniani ya mafanikio ya kiteknolojia ya binadamu ambayo yaliweka urithi mkubwa kwa maendeleo ya kiteknolojia.
Ni muhimu pia kutambua kuwa ukale wa bara la Afrika na namna ilivyotumia uwezo wake kwa mustakabali mzuri tunapopitia maendeleo ya ulimwengu wetu wa kisasa.
Busara ya kale
Tangu nyakati za zamani, Afrika iliweka msingi wa ustaarabu wa binadamu.
Katika jamii za kizamani za Kiafrika, mababu zetu waligundua vitu tofauti ambavyo vinabaki kuwa muhimu hadi leo.
Kwa mfano, Wamisri, ambao walitunga vitabu vya hisabati vilivyo na dhana ambazo bado ni za msingi kwa mifumo yetu ya elimu.
Ujuzi wao wa katika njia za kijiometri, kuelewa hesabu za algoriti kama vile pi, na uzuri wa usanifu ulioodhihirishwa katika ujenzi wa mapiramidi unaoneshwa uwezo mkubwa wa Afrika kiakili.
Afrika ndio chanzo cha unajimu na hisabati.
Pengine, ujenzi wa kale zaidi kufanywa na mwanadamu ni mwanadamu wa kale zaidi ni miduara ya mawe ya kalenda ya Adamu huko Afrika ya Kusini.
Miaka kama 44,000 iliyopita, vijiti vya kuhesabu na mifupa ndivyo vilivyotumika badala ya vikokotozi.
Zaidi ya hayo, watu wa Dogon wa Mali wanasalia kuwa na msukumo katika uelewa wao wa hali ya juu wa miili ya mbinguni, ambayo bado inaongeza changamoto ya ufahamu wa kisasa.
Bara la Afrika bado linaonekana kuwa kinara katika sekta tofauti kama vile kilimo na tiba.
Katika tiba, dawa na mimea ya kienyeji na ya kale, ilitumika na inaendelea kutumika na madaktari hata leo.
Ujuzi wa chanjo dhidi ya ndui umejulikana kwa watu wa Akan kutoka Afrika Magharibi.
Kwa upande wa kilimo, sekta hiyo ilianzia kwenye kingo za Mto Nile.
Urithi uliofichika
Tofauti na dhana zilizotawala, Afrika ilikuwa chimbuko la uvumbuzi tofauti kabla ya utawala wa kikoloni.
Kuenea kwa haraka kwa ujenzi ya kisasa ya kilimo, ufundi wa chuma, na maajabu ya usanifu. Ufundi kama vile ujenzi wa mashua unaofanywa na watu wa Mali na Songhai
Boti, ambazo zilikuwa na uwezo wa kustahimili misukosuko ya baharini sawa na ukubwa wa boti za Viking, zilikuwa muhimu kwa uvuvi, biashara, na mawasiliano kando ya mwambao na mito.
Pamoja na maendeleo haya, ujio wa kikoloni ulisababisha mwenendo mgumu wa kiiteknolojia.
Teknolojia mbalimbali kama vile telegrafu, reli, meli za mvuke na bunduki zilianzishwa.
Hata hivyo, teknolojia hizi zilitumika kimkakati na mara nyingi zilitumika kuvuruga na kuzuia maendeleo ya kiasili.
Teknolojia hizi za kigeni kulivuruga mazoea ya jadi, na kusababisha shida za kijamii na kiuchumi.
Enzi hizi zilishuhudia uanzishwa kwa teknolojia fulani, athari ya jumla ilihusisha mchanganyiko wa unyonyaji, uharibifu, na kukabiliana na hali ambayo ilifungua njia ya matatizo na fursa zilizopatikana katika nyakati za baada ya ukoloni.
Baada ya uhuru, Afrika ilikabiliwa na changamoto na fursa tata, na kuathiri mwelekeo wake wa kiteknolojia.
Baada ya utawala wa kikoloni, mataifa mapya yaliyojitegemea yalijishughulisha na kujenga miundombinu imara na uwezo wa kiteknolojia.
Nchi nyingi zimepiga hatua kubwa katika kuboresha elimu na uvumbuzi, na kukuza kizazi cha wataalamu wenye ujuzi.
Hata hivyo, tofauti za kiuchumi zinazoendelea na ukosefu wa utulivu wa kisiasa ulileta vikwazo kwa maendeleo makubwa na yaliyoenea ya teknolojia.
Japo kumekuwa na maendeleo, masuala kama vile mgawanyiko wa kidijitali na kuhakikisha ufikiaji jumuishi wa teknolojia bado ni kazi muhimu ya kuonesha uwezo wa Afrika kiteknolojia.
Jambo la kuruka
Kimsingi, hii inamaanisha maendeleo ya haraka au kuruka hatua za kawaida za maendeleo au teknolojia. Maandeleo ya kiteknolojia barani Afrika ni ushahidi tosha wa maajabu ya hatua huu kubwa.
Safari ya bara hili, hasa katika masuala ya mabadiliko ya kidijitali kama vile teknolojia ya simu za mkononi, inadhihirisha uwezo wake wa kusonga mbele zaidi.
Huku ikiangazia utumizi mkubwa wa simu mahiri, inasaidia pia tasnia zingine ambazo ziko tayari kukua katika nyanja za kijamii na kiuchumi.
Kulingana na ripoti ya hivi karibuni Afrika ambayo inatathmini mifumo ya uchumi ya kidijitali ya mataifa, Kenya na Afrika Kusini zinaongoza katika mabadiliko ya kidijitali, zikifuatwa na Nigeria, Misri, Rwanda na Ethiopia.
Kila nchi ina uwezo wake wa kipekee na changamoto katika safari yake ya kidijitali.
Kenya na Afrika Kusini zinalenga kuinua sekta mahususi kama vile kuunda kazi za kidijitali na uhuru wa kidijitali ili kuwa na ushindani katika soko la kimataifa.
Faida na hasara za mapinduzi ya teknolojia Afrika
Pengine, suala la muhimu hapa ni utayari wa bara la Afrika katika kupokea mabadiliko.
Tofauti na maeneo mengine ya kiuchumi yaliyoimarika zaidi, Afrika imeruhusu miamala ya fedha kupitia simu za mikononi, ambazo zimelifanya bara hili kupata maendeleo ya kiuchumi.
Hatua hiyo ilichochea harakisha athari nyingi za haraka, kutoka huduma za kibenki kwa njia ya simu hadi kwenye nishati mbadala zinazorahisisha maisha.
Mabadiliko haya, yalifungua fursa za ajira, masoko na mengineyo.
Katika ulimwengu unaoendelea kwa kasi wa teknolojia ya kimagharibi, watu ama wanatikisa mambo au wanatikiswa.
Hata hivyo, kupitia kuanzishwa kwa viatamizi tofauti barani Afrika, wafanyabiashara hawana uhuru wa kuvuruga au kusababisha machafuko kwani hakuna nyenzo zilizoanzishwa kufanya hivyo.
Badala yake, lazima watengeneze kitu kipya kwa kutoa bidhaa au huduma ambayo haijaonekana hapo awali ili iweze kuigwa na wengine.
Pamoja na maendeleo haya, ni vyema kutambua na kukabiliana na changamoto za utawala bora barani Afrika.
Changamoto hizi pia zimesababisha suala la kudumu la upungufu wa kufikiri wenye kutishia uwezo wa Afrika.
Ili kuinua akili ya watu wake, Afrika lazima izingatie kukuza uchumi wake, huduma za afya, kilimo, miundombinu, na mifumo ya utawala ili kuzuia watu wenye talanta kuhamia ughaibuni.
Mategemeo yajayo
Ukuaji wa sasa wa Afrika unaiweka kama soko ambalo halijatumika, na wawekezaji hakika wanatazamia bara hili kama nafasi ya uvumbuzi wa teknolojia.
Bila shaka, sekta binafsi itaendelea kusukuma gurudumu la maendeleo la uchumi wa bara la Afrika.
Ushirikiano unaokua wa Afrika na mataifa mashuhuri wa BRICS unatoa manufaa ya kuahidi kwa maendeleo ya kiuchumi na kiteknolojia, ambayo ni pamoja na makubaliano ya ujenzi wa nishati endelevu, viwanda, kilimo-hai, mfumo dhabiti wa kitaasisi, biashara, na ushirikiano wa kimataifa.
Utayari wa bara hili kuchunguza suluhu za kibunifu za kifedha pia unaonyeshwa na mataifa kama vile Senegal na Tunisia, ambazo juhudi zake za kuanzisha sarafu za kidijitali zenye msingi wa blockchain zinaashiria hatua muhimu.
Hii inaonesha kupitishwa kwa haraka kwa bara na hamu kuelekea mfumo wa hali ya juu wa kifedha.
Safari ya Afrika kufikia mapinduzi ya Kidijitali ina akisi uthabiti na ustahimilivu na uwezo wake ambao bado haujatumika ipasavyo katika kuifanya teknolojia kama nyenzo ya maendeleo jumuishi.
Hii itadhihirisha simulizi mpya ambayo itaongoza ulimwengu kutambua michango ya zamani ya Afrika na kukumbatia uwezo wake wa kuunda mustakabali mzuri unaoendeshwa na teknolojia.