Unicef inasema kuwa watoto milioni 40 walijiunga na nguvu kazi katika miaka minne iliyopita. / Picha: Getty Images
Na FirmainEric Mbadinga
Akiwa njiani kuelekea nyumbani baada ya siku ya kazi ngumu, jambo lenye umuhimu pekee kwa Jean Ralph Odzaga ni jinsi basi litakavyomfikisha anapokwenda kwa haraka.
Joto jingi, msongamano, kelele za abiria wengine, mlio wa honi za magari njiani - yote ni mepesi ikilinganishwa na uchovu unaomshinda fundi huyu wa ujenzi huko Libreville, Gabon.
Siku hiyo ilikuwa tofauti, karibu kama mshtuko. Jean alikuwa amechoka kama kawaida, lakini kuona wanandoa wakijaribu kuwatuliza watoto wao wawili kati ya watatu waliokuwa ndani ya basi lililokuwa na watu wengi, ilikuwa vigumu kupuuza.
Wavulana hao wawili, wenye umri wa mwaka mmoja na miaka mitatu hivi, walipokuwa wakipiga kelele, macho ya Jean yalimlenga mtoto mkubwa. Alikuwa msichana mwenye umri wa miaka mitano hivi. Alikuwa kimya na uso wake ulikuwa na hisia.
Mwanamke aliyeketi kando na Jean alikuwa akimtazama msichana huyo kwa makini kama yeye. Alipumua kwa nguvu kabla ya kusema, " Msichana Maskini! Tuko katika hatari ya kumwibia mtoto huyu utoto wake."
Jean alishangaa. "Niliendelea kumuuliza mwanamke huyo alimaanisha nini kwa hilo," ameiambia TRT Afrika.
"Alitoa nadharia kwamba inawezekana msichana mdogo hakupata msaada aliohitaji kwani wazazi wake walikuwa wakishiriki pakubwa katika kutunza watoto wawili, labda bila msaada wowote nyumbani. Hata anaweza kuwa msaidizi kwa kaka zake akiwa na umri mdogo."
Jean alipomuuliza jinsi alivyoweza kuwa na uhakika kwamba ndivyo ilivyokuwa, abiria mwenzake alisisitiza kwamba ilikuwa "uwezekano" tu. Kisha akashuka kwenye basi.
Jean alielewa siku hiyo kile ambacho watu wengi wanaweza kufahamu lakini hawaoni ni nini: ukweli wa "utoto ulioibiwa."
Kuanzia zama za kati hadi leo, na kutoka Afrika hadi ulimwengu mzima, ustawi wa akili na mwili wa watoto ni mada ambayo imebadilika, na kuvutia umakini zaidi.
Mantiki ya kuwafanya watoto wenye umri wa miaka 5 hadi 16 wafanye kazi ngumu katika maduka au mashamba wakati mmoja ilikuwa ya kawaida, angalau hadi mwisho wa karne ya 18, hasa maeneo ya Magharibi.
Ili kuhakikisha kwamba watoto wote ulimwenguni wanaweza kufurahia utoto wao na kupata elimu na utunzaji bora, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilianzisha Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto ( UNICEF) mnamo 1946.
Dkt. Comlan Kouassi, Mwanasaikolojia mjini Cotonou, Benin, anaashiria suala la utoto ulioibiwa kama shida ya kijamii ambayo ina athari kubwa kwa ukuaji wa akili na utu uzima baadaye.
"Tukiwa watoto, ni wakati wa kujifurahisha, kutegemea watu wazima. Tunahitaji pia kujizoesha na kujiandaa kwa maisha ya utu uzima. Lakini katika nchi nyingi za Afrika, ikiwemo Cotonou hapa Benin, watoto wengi wanapaswa kufanya kazi ili kujitegemea," anaiambia TRT Afrika.
Watoto wengine hata wanapaswa kufanya kazi ili kuwasaidia wazazi wao, huku wakikosa kile kinachopaswa kuwa utoto usio na wasiwasi.
"Wanalazimika kuishi kama watu wazima. Ningeita jambo hili 'uzazi wa watoto.' Licha ya kuwa watoto, wanapaswa kutafuta riziki yao ya kila siku," anasema Dkt. Kouassi.
Kulazimishwa kuwa mtu mzima
Utu uzima wa kulazimishwa
Jack De Souza, raia wa Togo mwenye umri wa miaka 17, ni msusi huko Lomé. Ni taaluma ambayo Jack anafanya kwa kusita kwa sababu ya hali yake ya maisha.
Baada ya kuachwa na wazazi wake alipokuwa na umri wa miaka 12, Jack hakupata utoto wa kawaida. Anadai kuishi kwake katika kituo cha mapokezi cha Watoto cha Kpa Domeviwo, ambacho kilimsaidia katika miaka yake ya awali.
"Hata Baada ya kupata riziki kupitia ususi, Jack anasema anahisi upweke ambao mara nyingi humshinda.Baada ya kujilea mitaani kufuatia kukataliwa na wazazi wangu bila kuelezewa, ilibidi nipate ujuzi wa ususi ili kujitegemea. Ninapoona watoto kama mimi na wazazi wao, ninahisi unyonge. Lakini hayo ni maisha," anasimulia.
Wanasayansi wa kijamii wanapendekeza kwamba watoto wengine hawapati malezi ya kawaida kwa sababu za kiuchumi. Kuvunjika kwa muundo wa familia kunachukuliwa kuwa mojawapo ya sababu zinazochangia jambo hili.
"Kuachwa kwa hiari kwa wazazi pia ni jambo la kawaida," anasema Dkt. Kouassi. "Katika visa vya wazazi kujiondoa au umaskini, baadhi ya watoto wanalazimika kuomba."
Hatari zisizoonekana
Kulingana na Consortium forStreet Children, Shirika la kuwasaidia watoto, watoto walioachwa, mara nyingi huathiriwa na "kudhulumiwa kingono, kimwili, au kihisia, na maradhi kama HIV/UKIMWI." Wengine wanavutiwa na uhalifu, na wengine wanakabiliwa na changamoto za afya ya akili.
Emmanuel Dogbevi Kutoka Ghana hakuishia mitaani kama Jack kutoka Togo, lakini ukuaji wake ulikuwa mgumu baada ya wazazi wake kutengana.
"Nilikulia na mama mmoja. Tulikuwa tisa, na ilikuwa ngumu," anakumbuka.
"Baada ya kumaliza shule ya msingi mwaka wa 1983, nikiwa na umri wa miaka 15, niliombwa nitafute kazi. Ndio sababu ilinichukua muda mrefu kupata elimu yangu ya juu. Niliingia chuo kikuu nikiwa na miaka 31," anaiambia TRT Afrika.
Emmanuel, ambaye sasa ni mwanahabari mpekuzi maarufu nchini Ghana, anaweza kuwa tofauti. Utoto ulioibiwa mara nyingi huwa na uchungu usiopona.
Mkataba wa Umoja wa Mataifa juu ya Haki za Mtoto, ambao umepitishwa na karibu kila nchi mnamo 2002, unawahakikishia watoto haki saba za msingi.
Nchi zilizotia sahihi mkataba huo lazima zihakikishe kwamba kila mtoto ana familia (ya kibiolojia au ya namna nyingine), elimu, shauku, makazi, tafrija, na utunzaji.
Kwa bahati mbaya, mengi ya haya bado hayajatekelezwa.
Kulingana na Unicef, katika Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara, ukuaji wa idadi ya watu, umaskini uliokithiri, na hatua za kutosha za ulinzi wa kijamii ni sababu za takriban watoto milioni 16.6 kujiunga na nguvu kazi katika miaka minne iliyopita. Jumla ya idadi hiyo ni karibu milioni 40.