Serikali ya Rwanda inaendelea kukana kushikiriana na waasi wa M23. /Picha: Wengine

Ubalozi wa Rwanda nchini Uingereza umetoa tamko rasmi kufuatia kutakiwa kutoa maelezo na Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo, ikielezea kuongezeka kwa wasiwasi wa kiusalama na hali tete ya mgogoro unaoendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Taarifa iliyotolewa na ubalozi inatilia mkazo mtazamo wa Rwanda katika hali ya usalama na kuitaka Serikali ya Uingereza kuungana na vikosi vya kutafuta amani vinavyoungwa mkono na Umoja wa Afrika.

Taarifa hiyo pia imesema kuwa, Jeshi la Rwanda linachukua hatua za kujilinda kufuatia tishio la usalama.

Hii inafuatia tukio la hivi karibuni ambapo katika mji wa Rubavu uliopo mpakani, watu 16 walipoteza maisha huku raia 177 wakijeruhiwa, kama ushahidi wa tishio la usalama.

Kauli hii ya Rwanda, inafuatia kuitwa kwa Balozi wa Rwanda nchini Uingereza baada ya nchi hiyo kudai Jeshi la Rwanda pamoja na vikosi vya M23 vimekuwa vikielekea mashariki mwa DRC.

Katika taarifa yake, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Uingereza amenukuliwa akisema, “Serikali ya Rwanda lazima iondowe vikosi vyake vyote haraka iwezekanavyo kutoka ardhi ya DRC.”

Rwanda siku zote imekuwa ikikana kuhusishwa na M23.

TRT Afrika