Mwezi Machi mwaka jana, DJ Joozey alikuwa mtu wa kwanza kupiga muziki kwa dakika 15 kwenye kilele cha mlima KIlimanjaro./Picha: Bongo5.com

Kila mwaka, maelfu ya watu hupanda mlima Kilimanjaro, ambao ni mrefu kuliko yote Afrika.

Kati yao, wapo wanaofanya hivyo kama fahari, na wengine huamua kukwea mita 5,895 kama sehemu ya kujiwekea historia muhimu kwenye maisha yao.

Mmoja wao ni DJ Joozey ambaye, mnamo mwezi wa tatu mwaka jana, aliamua kupanda na vifaa vyake hadi kwenye kilele cha Uhuru, na kupiga muziki.

Mwezi Juni mwaka 2017, timu mbiili za wanawake zilicheza mpira juu ya mlima huo, na kuweka rekodi ya dunia ya kucheza mpira kwa dakika 90 kwenye urefu wa futi 19,000./Picha: climbkilimanjaroguide.com

Changamoto tofauti ikiwemo ya hali ya hewa, hususani mgandamizo wa hewa katika maeneo ya mlima huo, hufanya shughuli ya upandaji kuwa pevu zaidi.

Hata hivyo, wapo walioweza kushinda changamoto kama hizo, na kuamua kucheza mpira kwenye mlima huo.

Kati ya wachezaji hao 30 kutoka mataifa zaidi ya 20 duniani pia walikuwepo nyota kama nyota wa zamani wa Marekani Lori Lindsey na mchezaji wa zamani wa Uingereza Rachel Unitt.

Siobhan Brady kutoka Ireland aliweka rekodi ya dunia kwa kupiga kinubi juu ya Mlima Kilimanjaro mwaka 2023./Picha:TANAPA

Mpiga kinubi huyo aliweka rekodi mpya ya Guinness baada ya kufanya onesho la dakika ishirini, akitumia kinubi chake, kwenye kilele cha juu kabisa barani Afrika .

Hii ilikuwa ni sehemu yake ya kusaidia wale wanaoishi na ugonjwa wa cystic fibrosis.

Cystic fibrosis ni ugonjwa wa kurithi ambao huunda kamasi nene ambazo hunata nata hasa kwenye mapafu na kongosho.

Kyle Maynard alikuwa mlemavu wa kwanza duniani, asiye na mikono wala miguu kupanda mlima Kilimanjaro, Januari 15, 2012./Picha:Kyle Maynard

Moja ya sifa ya kuupanda Mlima Kilimanjaro ni utimamu wa kiakili na kimwili. Hata hivyo, Kyle Maynard mtunzi wa vitabu na mtoa hamasa kutoka Marekani alipanda mlima Kilimanjaro kwa 'kutambaa', bila msaada wa vifaa vyoyote.

Mlemavu huyo alitumia siku 10 tu, katika kuweka rekodi hiyo.

Kwa kawaida, upandaji wa Mlima Kilimanjaro, kwa mtu mwenye afya njema, hutumia kuanzia siku tano hadi tisa, kupanda mlima Kilimanjaro, kutegemea na njia itakayotumika.

Akiwa na The Republic 89, Anne Lorimor alikuwa binadamu mzee zaidi kufika kileleni mwa Mlima Kilimanjaro. Hiyo ilikuwa Julai 12, 2019./Picha: The Republic

Anne Lorimor aliithibitishia dunia kuwa umri si kitu chochote bali ni namba tu baada ya kuonesha ujasiri na ushupavu wa kupanda Mlima mrefu kuliko yote Afrika.

Lorimor, kutoka Marekani alitumia njia ya Rongai, mojawapo ya njia za mbali na yenye kufunikwa na msitu.

Karl Egloff alipanda mlima Kilimanjaro kwa 'kukimbia' ndani ya saa 4 na dakika 56./Picha: rxrsports.com

Pengine hii ndio rekodi ya kushtua na kushangaza zaidi. Wakati waongoza utalii Mlima Kilimanjaro husisitiza neno 'polepole' wakati wote wa kukwea moja ya vilele 7 duniani, mwanariadha Karl Egloff mwenye uaria wa Uswiswi na Ecuador aliamua kukimbia kuelekea kileleni ndani ya saa 4 na dakika 56 tu.

TRT Afrika