Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud ameapa kupambana na magaidi katika eneo la Pembe ya Afrika.
Akizungumza siku ya Jumatatu jijini Mogadishu, wakati wa ufunguzi wa hospitali mpya ya Hodan, Rais Mohamud alipongeza hatua ya hivi karibuni ya Marekani ya kufanya shambulizi la anga dhidi ya magaidi wa Daesh katika eneo la Puntland.
Amesema kuwa hatua hiyo ya utawala wa Trump inadhihirisha nia ya pamoja ya kuondoa vitisho vyote dhidi ya amani ya Somalia.
Siku ya Jumatatu, Kamandi ya Afrika ya Jeshi la Marekani (AFRICOM) lilithibitisha kutekeleza mashambulizi ya anga dhidi ya Daesh na Somalia.
Lilikuwa shambulio la tatu la anga katika kipindi cha miezi miwili.
Zaidi ya magaidi 30 waliuwawa katika shambulio la anga kaskazini mwa jimbo la Puntland Jumatano iliyopita.