Rais wa Kenya William Ruto amehutubia taifa akiongelea maandamano yanayoendelea dhidi ya serikali. Ruto awataka upinzani kusitisha maandamano ya kila wiki ya kupinga serikali.
Maandamano hayo nchini Kenya yameongozwa na mkuu wa muungano wa AZimio Raila Odinga. Sababu za maandamano ni pamoja na gharama ya juu ya maisha nchini na madai ya upinzani kwamba matokeo ya kura za kitaifa za 2022 yaliyompendelea Rais William Ruto yalikuwa na utata.
Serikali inaripoti kuwa takriban watu 3 wameuawa katika maandamano hayo na mamia kujeruhiwa wakiwemo maafisa wa usalama.
Maeneo mawili ya ibada yameteketezwa na baadhi ya biashara kuporwa wakati wa maandamano hayo ambayo yamepangwa kufanyika kila Jumatatu na Alhamisi na upinzani.
TRT Afrika