Serikali itasimamia gharama za matibabu kwa wote waliojeruhiwa na pia gharama za mazishi / Picha : X- Chalamila 

Rais wa Tanzania Samia Suluhu ameagiza vyombo husika kufanyia uchugnuzi mijengo yote ya kibiashara jiijini Daresalaam hasa katika eneo la Kariakoo ambako biashara nyingi hufanyika.

Rais Samia pia aliwataka wananchi kuwa na ustahamilizu akiwahakikishia kuwa shughuli ya uokoaji inaendelea vyema na kuwa waokoaji wana imani kuwafikia wale bado wamenaswa chini ya vifusi.

Takwimu zinaonyesha kuwa waliofariki wamefikia 13 huku zaidi ya watu 80 wakipokea matibabu na wengine kuachiliwa kwenda nyumbani.

Pia Rais Samia alitoa ahadi kuwa serikali itasimamia gharama za matibabu kwa wote waliojeruhiwa na pia gharama za mazishi.

''Namtaka Waziri mkuu aongoze timu ya wakaguzi majengo, waendelee na zoezi la kukagua eneo lote la Kariakoo na tupate taarifa kamili ya hali ya majengo ya Kariakoo ilivyo,'' amesema Rais Samia.

Rais Samia alikuwa akihutubiakatika video kwenye mtandao wa X, akiwa nchini Brazil kuhudhuria kikao cha G20.

Katika hotuba hiyo, Samia pia aliagiza jeshi la polisi kuchukua maelezo kamili ya wamiliki wa jengo lililoporomoka, kandarasi zao za ujenzi sababu na kuporomoka, ambapo matokeo yatawekwa wazi kwa umma.

Jengo la ghorofa nne liliporomoka Jumamosi asubuhi na kuwauwa watu 13 huku wengine zaidi ya themanini wakitolewa wakiwa na majeraha mbali mbali.

Shughuli ya uokoaji bado inaendelea na inaaminiwa kunao ambao bado wamenaswa chini ya vifusi.

TRT Afrika