oKiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga | Photo: AP / Photo: AFP

Muungano wa kisiasa wa Azimio One Kenya Alliance utaongozwa na timu ya kiufundi ya wanachama saba, kutokana na maamuzi ya kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, katika majadiliano ya pande mbili na serikali ya kutafuta muafaka kati yao.

Tımu hii ılızındulıwa wakati wa mkutano wa Azimio La Umoja One, Kenya kilichofanyika katika kaunti ya Machakos.

"Tunakubali kwamba hatua bora zaidi ni mchakato wa haki utakaongozwa na wabunge kutoka pande zote mbili na kuungwa mkono na wataalamu. Baada ya hapo, yatawasılıshwa bungenı ılı kuidhinishwa na Bunge.’ Alısema Raila.

Timu hıı ılıyochagulıwa ımeıbua hisia za kurudi nyuma katika kile kilichoonekana kuwa ni Raıla Odınga kujiondoa kwa matakwa yake ya awali ya kutaka mazungumzo sawa na makubaliano ya Sheria ya Ukweli, Haki na Maridhiano ya 2008.

Alitoa kile alichotaja kuwa viwango vya chini vya matakwa visivyoweza kupunguzwa ambavyo vilipaswa kujadiliwa katıka mazungumzo hayo.

“Tunaingia kwenye mazungumzo haya tukiwa na imani thabiti kwamba matakwa yetu ni ya haki, nia yetu ni safi na lengo letu ni la kizalendo. Tunaingia kwenye mazungumzo haya tukiamini kwamba baadhi ya masuala, hasa ya kupunguza bei ya chakula, ni ya dharura, hayawezi kusubiri na hata hayahitaji mazungumzo,” Odinga alisema.

Madai yake mengine ni pamoja na ukaguzi wa kitaalamu wa seva zinazotumiwa na tume ya uchaguzi nchini Kenya, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), kabla, wakati, na baada ya uchaguzi uliokuwa na upinzani mkali wa 2022, ushiriki wa upinzani katika uteuzi wa wakuu wa IEBC, na kupitishwa kwa sheria zıtakazoshughulikia mapungufu ya uchaguzi, utawala na uchumi yaliyogunduliwa wakati wa uchaguzi.

Hata hivyo, Rais William Ruto alisema kwa kupinga ombi la Raila la mazungumzo sawa na ya Sheria ya Ukweli, Haki na Maridhiano ya 2008 akitangaza kwamba hatashiriki katika mijadala kama hiyo.

"Mazungumzo ya ubinafsi kwa wanasiasa yalimalizika baada ya uchaguzi wa mwaka jana," alisema Rais Ruto.

“Tunaingia kwenye mazungumzo haya tukiwa na imani thabiti kwamba matakwa yetu ni ya haki, nia yetu ni safi na lengo letu ni la kizalendo. Tunaingia kwenye mazungumzo haya tukiamini kwamba baadhi ya masuala, hasa ya kupunguza bei ya chakula, ni ya dharura, hayawezi kusubiri na hata hayahitaji mazungumzo,” Odinga alisema.

Raila Odinga
TRT Afrika na mashirika ya habari