Watu wakitembea katika barabara baada ya polisi kukabiliana na magenge ya wahalifu mjini Port-au-Prince, Haiti Februari 23, 2025. / Picha: Reuters

Afisa mmoja wa polisi wa Kenya aliyekuwa katika kikosi cha kukabiliana na magenge ya wahalifu nchini Haiti ameuawa wakati wa makabiiano hayo, Mamlaka nchini Kenya zimesema siku ya Jumapili.

Alipigwa risasi na kuuawa katika eneo la Artibonite magharibi, ambapo polisi wa Kenya waliopelekwa kukabiliana na magenge ya wahalifu walikuwa wakiendesha operesheni zao kwa wiki nzima.

Huyu ni afisa wa kwanza kuuawa miongoni mwa vikosi vinavyoongozwa na Kenya ambavyo viliwasili nchini humo Juni 2024 kwa lengi la kuhakikisha hali ya usalama.

"Tunatia heshima zetu kwa shujaa wetu aliyefariki," Jack Ombaka, msemaji wa ujumbe huo, alisema kwenye taarifa. " Tutakabilana na haya magenge ya wahalifu hadi pale tutakapowamaliza wote. Hatutokuangusha."

Kuongezeka kwa vurugu

Kikosi hiko cha Kenya kimesema kwenye taarifa kuwa maafisa wake walikuwa wameenda kuwasaidia wakazi wa eneo la Pont-Sonde.

Mauaji ya Jumapili yamejiri huku kukiwa na ongezeko la vurugu katika sehemu ya mji wa Port-au-Prince katika wiki moja iliyopita.

Polisi alichukuwa kwa helikopta kutoka sehemu na akafariki baadaye kutokana na majeraha, Godfrey Otunge, kamanda wa kikosi cha Kenya nchini Haiti, alisema katika taarifa.

Baada ya kupigwa risasi, polisi walikabiliana na majambazi hao. Afisa wa ujumbe huo Ombaka aliwashkuru wahudumu wa hospitalina vikosi vya El Salvador ambavyo pia vinakabiliana na magenge hayo ya wahalifu kwa msaada wao baada ya tukio hilo.

“Hivi ndivyo namna shujaa alivyojitolea — aliuawa wakati akipigania watu wa Haiti,” Ombaka alisema katika taarifa. “Tunatoa heshima zetu kwa shujaa huyu aliyeuawa."

Pigo kwa vikosi hivyo

Maafisa walitoa taarifa zaidi, lakini genge la Gran Grif linadhibiti eneo hilo.

Kifo chake ni pigo kubwa kwa jitihada na kukabiliana na magenge ya wahalifu ya Haiti, ambayo yametikisa nchi hiyo tangu alipouawa Rais Jovenel Moïse 2021.

Kenya imepeleka mamia ya maafisa huko kusaidia maafisa wa usalama ambao wanasuwasuwa nchini Haiti.

Mwezi Februari, maafisa 200 zaidi wa polisi kutoka kwa taifa hilo la Afrika Mashariki walipelekwa kuungana na maafisa 600 zaidi ambao tayari walikuwa wanafanya kazi pamoja na maafisa wa polisi wa Haiti ikiwa sehemu ya vikosi vya kimataifa wakisaidiwa na wanajeshi na polisi ikiwemo kutoka Jamaica, Guatemala na El Salvador.

TRT Afrika na mashirika mengine

Reuters