Bobi Wine aliwaambia waandishi wa habari akiwa ndani ya nyumba yake kwamba aliwekwa chini ya ulinzi. Picha: Getty

Polisi nchini Uganda imetoa taarifa na kujiondolea lawama dhidi ya mwanasiasa wa upinzani ambaye pia ni msanii maarufu nchini humo Robert Ssentamu Kyagulanyi maarufu Bobi Wine na kupinga kumkamata.

Hii ni baada ya chama cha kiongozi mkuu huyo wa upinzani nchini Uganda, Bobi Wine, kusema kuwa kiongozi wao alilazimishwa ndani ya gari na maafisa wa usalama wa Uganda na kupelekwa nyumbani siku ya Alhamisi baada ya kushuka kutoka kwenye ndege akirejea kutoka safari ya nje ya nchi.

Tunataka kuufahamisha umma kuwa rais wa NUP, Robert Kyagulanyi alifanikiwa kuandamana na kikosi chetu cha usalama kutoka uwanja wa Entebbe hadi kwake Magere. Alifika nyumbani kwake karibu saa 11: 20 asubuhi, na yuko na familia yake na marafiki.

Bobi Wine aliwaambia waandishi wa habari akiwa ndani ya nyumba yake ya kwamba alikuwa amewekwa chini ya kifungo cha nyumbani.

Msemaji wa Polisi Uganda SSP Patrick Onyango. Picha: Polisi wa Uganda

"Kama tunavyozungumza hivi sasa, niko chini ya kifungo cha nyumbani," alisema. "Kwa sababu nyumba yangu imezungukwa. Askari na polisi wako katika sehemu zote.”

Polisi wa Uganda walipuuza madai hayo

Puuzeni uvumi wa kukamatwa kwake (Bobi Wine) na waenezaji porojo. Wakati huo huo, shughuli za biashara na harakati kando ya Barabara ya Entebbe, ndani ya Kampala na Gayaza, zinaendelea vizuri.

Mwanasiasa huyo wa upinzani ambaye pia ni msanii maarufu nchini Uganda aligombea urais mnamo 2021, bila mafaniko akishindwa na rais Yoweri Museveni katika uchaguzi aliodai ulikuwa umeibwa.

Aidha, siku ya jumatano, Polisi nchini Uganda walipiga marufuku shughuli za kumpokea Bobi Wine huku idara hiyo ikisema kuwa vyombo vya usalama vitawachukulia hatua wale wote watakaohusika katika shughuli isiyo halali watakamatwa na kufikishwa mbele ya mahakama za sheria.

"Mashirika ya pamoja ya usalama yamepokea habari za kuaminika zinazoonyesha kuwa kundi la wanaharakati wa kisiasa, wanaohusishwa na chama cha (NUP), wanaandaa na kuhamasisha wanachama wa umma kwa hafla iliyopangwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe mnamo oktoba 5, 2023, kumkaribisha rais wa NUP, Robert Kyagulanyi, ambaye anarudi kutoka nje ya nchi," Polisi ya Uganda ilisema.

Polisi imewataka wananchi kuacha kuandamana kwa madai kuwa kufanya hivyo, kunaweza kuvuruga amani, shughuli za watu, ikiwemo biashara.

TRT Afrika na mashirika ya habari