Mamlaka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta wamekamata zaidi ya kilo 1 ya dawa ya methamphetamine iliyofichwa ndani ya tandiko za baiskeli huku serikali ikizidisha vita dhidi ya ulanguzi wa dawa za kulevya.
Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ilisema Jumanne kwamba shehena hiyo ilikuwa ikielekea Jakarta, Indonesia.
"Wapelelezi wenye macho makali waliotumwa kwenye uwanja wa ndege ili kukabiliana na uhalifu wa wahamiaji na mizigo yenye kutiliwa shaka ilikuwa imekusanyika katika kibanda cha DHL kwa ajili ya zoezi la uhakiki, ambapo vifurushi vya rangi ya kahawia vilivyo na chumvu chumvi nyeupe juu yake vilipatikana vimefichwa kwenye viti vya baiskelo kumi na moja," DCI walisema katika taarifa na manahabari.
Baada ya kufanyiwa vipimo na uchunguzi zaidi, Mawakala walisema kuwa chumvi chumvi hiyo ilikutwa kuwa dawa iliyo haramu ya methamphetamine.
''Dawa hiyo inayokadiriwa kuwa zaidi ya Sh 9 milioni ilifichwa miongoni mwa bidhaa nyingine zilizotangazwa kuwa vifaa vya baiskeli katika shehena iliyokuwa ikisafirishwa kutoka Moroni, Comoro,'' taarifa hiyo ilisema.
DCI imesema kuwa Shirika la Polisi la Kimataifa la Uhalifu (INTERPOL) limeanzisha operesheni ya kuwasaka washukiwa wanaohusika na biashara hiyo haramu ili kukamatwa na kufunguliwa mashtaka.
Vita dhidi ya utumiaji wa dawa za kulevya na ulanguzi wa mihadarati na dawa nyingine haramu vimeshika kasi nchini Kenya, huku DCI ikionya kwamba: ''Ardhi ya Kenya itasalia kuwa uwanja wa chuki kwa wahusika wa dawa za kulevya, bila kujali hadhi yao nchini.''