Polisi nchini kenya inasema imemkata mtu ambaye anashukiwa kufanya mauaji ya wanawake ambao miili yao ilipatikana katika eneo la machimbo katika eneo la Mukuru kwa Njenga, katika eneo la Embakasi, jijini Nairobi.
"Leo mapema mwendo wa saa saba, tulimkamata mshukiwa wa mauaji haya, anaitwa Collins Jomaisi Khalisia," Douglas Kanja, Inspekta Mkuu Mtendaji wa polisi nchini kenya amewaambia wandishi wa habari.
Khalisi anadaiwa kuutupa mwili wa mwathiriwa wake wa kwanza - mke wake - kwenye machimbo mnamo 2022.
"Tumepata mwili mmoja zaidi na kufikisha jumla ya miili 9 iliyopatikana hadi sasa. Uchunguzi wa miili unafanyika leo," Kanja ameongezea.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 33 alikamatwa katika klabu moja huko Kayole, na kupatikana akiripotiwa kuwa na kadi nyingi za simu .
Anashukiwa kuwaua waathiriwa, na kuweka miili yao katika mifuko ya plastiki na magunia na kuitupa katika machimbo hayo.
Kumekuwa na hisia tofauti kuhusu mauaji hayo huku wananchi wengine wakidai kuwa, huenda yalifanywa wakati wa mauaji na maafisa wa polisi.
Hata hivyo, Rais William Ruto aliwahakikishia Wakenya mwishoni mwa juma kuwa atahakikisha kuwa waliohusika katika mauaji hayo wanakamatwa na kuadhibiwa kisheria.