Waandamanaji hao wakipiga ngoma kwenye mitaa ya Johannesburg./Picha: AA

Na Sylvia Chebet

Kupitia mapigo iliyopangiliwa, waandamanaji hao wametumia ngoma 1,000 kama ishara ya kuiunga mkono Palestina, kwenye mitaa ya Johannesburg.

Wakilaani vita hivyo dhidi ya Gaza, waandamanaji hao wameitaka Jumuiya ya Kimataifa kuishinikiza Israel kusitisha mashambulizi hayo.

Jumla ya ngoma 1,000 zilitumika katika maandamano hayo./Picha: AA

Tukio la upigaji ngoma lilkuwa ni zaidi ya onesho la muziki. Ilikuwa ni njia ya kupaza sauti kuhusu janga la kibinadamu ambali halipaswi kufumbiwa macho.

Wapalestina wapatao 1,200 wamepoteza maisha tangu Israel ilipoanza mashambulizi dhidi ya Israel, Oktoba 7.

Takriban Wapalestina 32,000, wengi wakiwa watoto na wanawake wameuwawa katika eneo la Gaza, huku 74,200 wengine wakijeruhiwa katika machafuko hayo yanayoambatana na upungufu wa mahitaji ya muhimu ya kijamii.

Baadhi ya waandmanji hao./Picha: AA

Mwezi Januari, Mahakama ya Kimataifa ya Haki iliiamuru Tel Aviv kusitisha mauaji ya hayo ya kimbari na kuhakikisha upatikanaji wa msaada wa kibinadamu kwa raia wa Gaza.

Hii ni baada ya Afrika Kusini kuiburuza Israel katika mahakama hiyo kujibu mashitaka ya mauaji ya kimbari mjini Gaza. Hata hivyo, Israel imeendeleza mashambulizi hayo pamoja na uamuzi wa mahakama.

Waandamanaji wakionesha mshikamano kwa Palestina./Picha: AA

Sauti zilipazwa kulaani mateso ya watu wa Palestina pamoja na vivuli vya siku za nyuma, wakikumbuka miaka ya uchungu ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.

Watoto walikuwa ni sehemu ya tukio hilo./Picha: AA

Waandamanaji hao walikumbuka matukio ya Machi 21 1960, ambayo imekuwa siku ya Haki za Binadamu nchini Afrika Kusini ambayo pia ni Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ubaguzi wa Rangi.

Maandamano ya amani dhidi ya 'kupitisha sheria' za ubaguzi wa rangi zaidi ya miongo sita iliyopita yaligeuka kuwa mauaji ya kutisha wakati polisi waliwapiga risasi na kuwaua watu 69, wakiwemo watoto 29, na kuwajeruhi wengine zaidi ya 180.

Waandamanaji hao wakipiga ngoma kwenye mitaa ya Johannesburg./Picha: AA

Tarehe 21 Machi 1960 iliashiria mabadiliko makubwa katika historia ya Afrika Kusini kwani ilisababisha mapambano makali ya silaha kwa ajili ya ukombozi kutoka kwa ukatili na ukatili wa mfumo wa ubaguzi wa rangi wa wazungu wachache.

Imewahamasisha waandamanaji, kupitia ngoma 1,000 kwa ajili ya Palestina, kutoa wito wa kuchukuliwa hatua, huruma na uhamasishaji wa pamoja kwa ajili ya amani na utu kwa watu waliozingirwa wa Gaza.

TRT Afrika