Mpango wa Awa Keita Ndiaye umemaliza tatizo la kudumu la uhaba wa maji ambalo lilisumbua jamii Kaskazini mwa Senegal. / Picha: Awa Keita Ndiaye

Na

Firmain Eric Mbadinga

Awa Keita Ndiaye alikua huku akishuhudia familia yake ikikabiliana na uhaba wa maji wa muda mrefu, iwe wa kufuga ng'ombe au umwagiliaji wa mashamba.

Akiwa na umri wa miaka 26, anatumia shahada yake ya ujasiriamali wa kilimo kusaidia jamii yake katika kijiji cha Mbollo Aly Sidi nchini Senegali kukabilina na tatizo hili kufanikisha ufikiaji wa vyanzo vya maji usiokatizwa katika misimu yote.

Mpango wa Awa tayari umefanya mabadiliko. Tangu mwaka wa 2022, kijiji hiki kilichopo kati ya mikoa ya Podor na Matam kaskazini mwa Senegal kimekuwa kikipiga hatua kuelekea lengo la kuongeza tija yake ya kilimo na ufugaji kwa zaidi ya nusu.

Mradi wa Mbollo Aly Sidi ulianza huku Ada akilenga kuongeza upatikanaji wa maji kwa ajili ya umwagiliaji wa mashamba ya mababu ambayo ni mchanganyiko wa miti ya matunda, mahindi, mtama, mpunga na miwa. "Mateso ya familia yangu yaliniathiri sana. Niliamua mapema maishani kufanya jambo kuhusu hilo," anaiambia TRT Afrika.

Paneli za miale ya jua huwezesha mradi wa kusambaza maji kwenye madimbwi saba katika kijiji cha Mbollo Aly Sidi. / Picha: Awa Keita Ndiaye

"Mateso ya familia yangu yaliniathiri sana. Niliamua mapema maishani kufanya jambo kuhusu hilo," anaiambia TRT Afrika.

Mradi wa pamoja

Mradi uliofadhiliwa kwa pamoja unaohusisha wakazi wa eneo hilo na wabia binafsi, ulioanzishwa na mwanadada huyu umesababisha kupatika kwa mabonde saba ya maji katika eneo hilo kwa mahitaji ya jamii nzima.

Paneli za miale ya jua husaidia kutoa nishati na maji katika eneo ambalo hunyesha miezi mitatu tu kwa mwaka.

Mawimbi ya joto ya mara kwa mara, huku halijoto ikifikia nyuzijoto 40, iliongeza shida ya maji hadi mradi ulipopunguza matatizo ya jamii.

"Jumuiya ilichangia karibu asilimia 30 ya CFA 'franc' milioni moja na nusu zinazohitajika kwa mradi huo.

CorpsAfrica, mshirika wetu wa kibinafsi, ilitoa kiasi kilichosalia, ikiwa na uhakika wa umuhimu wa mradi huu.

Utekelezaji ulichukua miezi saba," anaeleza Awa.

Kuanzia mwanzo kabisa wa mpango huo hadi utekelezaji wake, sehemu moja muhimu ya safari ya mradi wa Awamu imekuwa ni ushiriki wa wanawake.

"Nilishuhudia shauku, furaha, kuridhika na kujivunia miongoni mwa wanawake na wanaume wa jamii yangu wakati mradi huo ukiendelea," anasema.

Wanawake wa kijiji cha Mbollo Aly Sidi waliamua kwamba mabwawa yajengwe kuzunguka masoko na maeneo ya bustani. /Picha: Awa Keita Ndiaye

Wasichana mstari wa mbele

Kwa kuzingatia mtazamo wa jumla wa mradi, wanawake 250 waliounda kikundi cha maslahi ya kiuchumi cha kijiji walifafanua eneo ambalo mabwawa saba yatajengwa.

Haishangazi, walichagua soko na maeneo ya bustani. “Mpango wa awali ulijumuisha uwekaji wa mfumo wa umwagiliaji wa mashamba kwa njia ya matone.

Hata hivyo, baada ya kufanya tathmini hatari zinazoweza kujitokeza, tulichagua fikra mradi endelevu. Kwa hiyo, tuliachana na mradi wa umwagiliaji kwa njia ya matone hadi mfumo wa kujenga mabwawa ya maji.

Kwa kile kilichosalia, tulinunua mitungi ya kumwagilia maji na paneli za miale ya jua," Awa anaiambia TRT Afrika.

Eneo kubwa la chemchemi hizi huruhusu mkusanyiko bora wa maji ikiwa vyombo vimejaa maji.

Kama ilivyo kwa chemchemi yoyote inayofanya kazi kwenye mfumo mmoja, maji kwenye bonde huzunguka kila mara na kuzalishwa tena.

Awa Keita Ndiaye, 26, ana shahada ya kwanza katika ujasiriamali wa kilimo. /Picha: Awa Keita Ndiaye

Tangu kuanzishwa kwake, wenyeji 1,680 wa Mbollo Ali Sidy wameweza kuongeza matumizi ya ardhi yao ya kilimo. Paneli za miale ya jua hutoa faida ya ziada.

''Baada ya muda, mipango mapya haya yote mpya yatawawezesha wanavijiji kupunguza nguvu kazi, kuokoa muda na nishati, na kuongeza mavuno. Katika suala kubwa zaidi, mradi unalenga kusaidia kuboresha usalama wa chakula," anasema Awa.

Malengo ni uzalishaji

Mradi unalenga kuwawezesha wakulima kuongeza uzalishaji kwa asilimia 80 katika mwaka mwingine na kuunda kundi kubwa la wanufaika wa moja kwa moja na wasio wa moja kwa moja wa shughuli hizi.

“Mradi huu umetuletea afueni kubwa hasa katika mapambano yetu ya kupata maji kwa ajili ya kilimo na mahitaji mengine kwa mwaka mzima, tunamshukuru na kumtakia Awa mafanikio zaidi,” anasema Kaw Moussa Mb Ali, kiongozi wa kijiji.

Awa ni mwanaharakati ambaye ana malengo makubwa. Dhamira yake mpya ni kuongeza ufahamu kuhusu elimu miongoni mwa vijana na wazazi wao huko Mbollo Aly Sidi kupitia kampeni ya kupunguza idadi wa wanafunzi kuacha shule.

TRT Afrika