Na Kevin Phillips Momanyi
Neno la Kiswahili "mitumba," tafsiri yake ni "vifurushi," humaanisha vifurushi vilivyofungwa vya plastiki vya nguo kutoka mataifa ya Magharibi.
Kila kitu katika soko hili hakika kinaweza kununuliwa kwa bei nafuu , ikiwa ni pamoja na nguo, viatu, chakula na vyombo.
Ukifanya makosa ya kuonyesha dalili ya "Mimi ni mpya hapa", wachuuzi watafanya kila wawezalo kukuuzia kwa bei ghali.
Wateja wanaweza kupata chapa yoyote maarufu ya kimataifa ya nguo au viatu katika duka lolote maarufu la London au maduka makubwa ya Ulaya yenye thamani kubwa kwa kutembelea soko la Gikomba la Nairobi.
Walakini, kuna jambo: nguo na viatu vyote ni vya mitumba. Gharama ya nguo na viatu vinaanzia $2 tu kwa kila moja na kuendelea.
Tanzania, Uganda, na Kenya ni miongoni mwa masoko makubwa zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kenya inaagiza karibu tani 100,000 za nguo zilizotumika kila mwaka.
Bidhaa za chakula pia zinauzwa huko.
Ingawa wasomi na maafisa wa serikali wanasema soko hili linaweza kuajiri mamia ya maelfu, ni vigumu kukadiria idadi kamili ya wanaonufaika kimaisha kutokana na soko hili.