Wakazi wanaoishi eneo lililoko karibu na mji mkuu wa Khartoum, Sudan wameamriwa kuhama, wenyeji walisema, huku mapigano kati ya jeshi na vikosi vya RSF yakiendelea kutikisa mji mkuu.
"Moto mkubwa wa mizinga" ulianguka kwenye maeneo yenye watu wengi katika mji mkuu wa Sudan na maeneo ya karibu, walioshuhudia waliambia AFP.
Karibu na Omdurman, mji pacha wa Khartoum wenye makovu ya vita, mizinga iliangukia nyumba za makazi.
Jeshi na vikosi vingine viliamuru kuhamishwa kwa raia kutoka Abu Rouf, kwa mujibu wa kamati ya upinzani ya kitongoji hicho, mojawapo ya makundi mengi yanayoandaa maandamano ya kuunga mkono demokrasia na yanayotoa msaada kwa familia zinazokabili moto.
Jeshi hilo lilifanya mashambulizi ya anga na kufyatua mizinga katika Daraja la Shambat ili kukata njia ya kuingia eneo hilo kutoka kwa maadui zao, Kikosi cha Kusaidia Haraka (RSF). Kundi la wanamgambo lilitumia daraja hilo kusambaza tena kutoka upande wa pili wa Nile, kulingana na mkaazi anayejadili uhamishaji huo.
Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), zaidi ya asilimia 80 ya hospitali za Sudan hazitumiki tena na tayari sehemu kubwa ya miundombinu ya nchi hiyo iliyokuwa tayari katika hali tete imeharibiwa.
Hali hiyo pia imesababisha "changamoto kubwa" kwa waathiriwa wa unyanyasaji wa kingono, ambao umekithiri wakati wa vita, "kupokea huduma muhimu za afya" Souleima Ishaq al Khalifa, daktari mkuu katika wakala wa serikali wa kupambana na ukatili dhidi ya wanawake, aliiambia AFP.
Tangu Aprili 15, Khalifa na wenzake wamenakili matukio 108 ya unyanyasaji wa kijinsia huko Khartoum na Darfur - eneo lenye machafuko la magharibi kwenye mpaka na Chad ambako robo ya watu milioni 48 wa Sudan wanaishi.
Idadi kamili huenda haikadiriwi, kama vile hasara za kibinadamu, kwani waathiriwa na walezi hawawezi kusafiri kwa sababu ya mzozo.
Waathirika wa ubakaji wanakabiliwa na mzigo maradufu, anaongeza, kwani "hakuna dawa tena huko Khartoum," na "huko Nyala (Darfur Kusini), hawawezi kufika hospitali kwa sababu kuna kambi ya RSF njiani".
Miji na vijiji vyote Darfur, kitovu cha mapigano yanayoendelea na ngome ya RSF vimeharibiwa, licha ya kuharibiwa katika miaka ya 2000 na vita vya wenyewe kwa wenyewe vya umwagaji damu.