Wakazi wa eneo la Darfur walikumbwa na ukosefu wa usalama hata kabla ya vita vipya vya Aprili 15 mwaka huu/ Photo: AFP

Shirika la kutetea haki za binadamu yaani, Human Rights Watch, imesema utafiti wake mpya unaonyesha kikundi cha Rapid Support Forces cha Sudan kiliua mamia ya raia huko Darfur Magharibi mapema Novemba 2023.

"Kundi la RSF walipora, kushambulia, na kuwazuilia kwa njia isiyo halali watu wa jamii ya Massalit huko Ardamata, katika kitongoji cha El Geneina Magharibi mwa Darfur," HRW ilisema katika taarifa.

Mnamo Aprili 15, 2023, mapigano katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum, kati ya Wanajeshi wa Sudan na Vikosi vya RSF, yalienea kwa kasi nchini kote.

Kiongozi wa Jeshi la Sudan Jenerali Abdelfattah al-Burhan na kiongozi wa RSF Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, anayejulikana kama "Hemedti," kwa pamoja walikuwa wamefanya mapinduzi dhidi ya serikali ya mpito ya nchi hiyo mnamo Oktoba 2021.

Kulingana na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), takriban watu 800 waliuawa wakati wa mashambulizi ya mapema mwezi Novemba huko Ardamata/ Picha: Reuters 

Vikosi vyote viwili vina historia ya kukiuka sheria za kimataifa za kibinadamu na haki za binadamu, haswa huko Darfur na wakati wa ukandamizaji dhidi ya waandamanaji.

Kulingana na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), takriban watu 800 waliuawa wakati wa mashambulizi ya mapema mwezi Novemba huko Ardamata.

Wanaopokea wakimbizi Chad walisema kutoka na mahojiani na waliokuwa wmetoroka vita,kati ya watu 1,300 na 2,000,waliuawa kutoak kwa eneo walilokuwa wakitoroka, ikiwa ni pamoja na kadhaa waliouawa kwenye barabara ya kuelekea Chad.

Takriban watu 8,000 wamekimbilia Chad, wakiungana na takriban 450,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, waliokimbia makazi yao kutokana na mashambulizi huko Darfur Magharibi hasa kati ya Aprili na Juni.

"Kwa kuzingatia kufungwa kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, na nafasi yake kuchukuliwa na mjumbe maalum, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linapaswa kufikiria kwa haraka njia za kuimarisha uwepo wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan ambazo zinaweza kuzuia ukatili zaidi na kulinda zaidi raia huko Darfur.

Shirika la HRW linasema ripoti yake imechangiwa kwa mahojiano na watu 20 wa jamii ya Massalit ambao walitorokea Ardamata mashariki mwa Chad kati ya Novemba 1-10.

Kati yao walikuwa wanajeshi watatu wa Jeshi la Sudan, ambao walielezea msururu wa mauaji, kushambuliwa kwa makombora, kuwekwa kizuizini kinyume cha sheria, unyanyasaji wa kingono, dhuluma na uporaji.

TRT Afrika