Mwili wa mwanafunzi wa Kitanzania aliyetoweka nchini Israel na kupatikana amefariki baada ya shambulio la Hamas mwezi Oktoba unatarajiwa kurejeshwa nyumbani leo Jumapili, familia yake imesema.
"Tulipaswa kupokea mwili Jumamosi, lakini kuna mabadiliko. Tunatarajia kupokea Jumapili, " Christina Mtenga, dada yake arehemu aliiambia AFP kwa simu Jumamosi.
Christina ameongeza kuwa mazishi ya nduguye yatafanyika siku ya Jumanne katika Nyumbani kwa familia, wilaya ya Rombo ilililoko eneo la Kilimanjaro, Kaskazini mwa Tanzania.
Imekuwa ni wiki ya majonzi kwa familia hiyo na wanafunzi wenza wa ndugu yake, kwani Clemence alipaswa kuhsiriki sherehe ya kuhitimu kutoka Chuo Kikuu cha Morogoro Mashariki Mwa Tanzania wiki hii.
"Ni hali ngumu lakini tunakabiliana," Christina alisema. "Clemence alikuwa mwenye adabu, mwenye bidii na jitihada nyingi. Alikuwa mtu wa dini na aliwapenda watu wengine."
Clemence Felix Mtenga 22, alikuwa mmoja wa Watanzania wawili walioathirika na shambulizi la kushtukizia la Oktoba 7 ambapo watu wasiopungua 240 walichukuliwa mateka, kwa mujibu.
Wizara ya mambo ya nje ya Tanzania ilithibitisha kifo cha Mtenga kupitia taarifa yake Novemba 18, bila kufafanua jinsi alivyouawa.
Clemence alifuzu baada ya kusoma shahada ya Ufugaji wa bustani.
Wizara ya mambo ya nje ya Tanzania imesema katika taarifa yake wiki iliyopita kwamba Mollel bado hajulikano aliko.