Uchaguzi huo umefanyika kufuatia  kuondoka kwa Harold Sungusia aliyemaliza muda wake./ Picha : TRT Afrika

WANACHAMA Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wamefanya Uchaguzi na kumchagua wakili msomi na maarufu nchini Boniface Mwabukusi kuwa rais wa chama hicho.

Mwabukusi ametangazwa mshindi wa kiti hicho kwa kupata kura 1,274 ambazo ni sawa na asilimia 63.1 dhidi ya washindani wake Sweetbert Nkuba, Revocutus Kuuli, Ibrahim Bendera, Paul Kaunda na Emmanuel Muga katika uchaguzi ambao kwa mara ya kwanza umefanyika nje ya Jiji la Arusha.

Kinyang'anyiro cha uchaguzi huo kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC) jijini Dodoma, kililenga kumpata mrithi wa Harold Sungusia aliyemaliza muda wake.

Matokeo ya uchaguzi huo yalitarajiwa kutangazwa saa 11 jioni, lakini yametangazwa saa 5. 15 usiku.

Matokeo yalichelewa kutangazwa tofauti na ilivyotarajiwa, kutokana na msiba wa mmoja wa wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho, Maria Pengo na kusogezwa muda kutokana na karatasi za kura kupungua

TRT Afrika