Mvua iliyonyesha kwa siku tatu iliharibu nyumba katika vijiji vya Kambamba na Bulape / Picha: AA

Mvua kubwa iliyonyesha imeharibu takriban nyumba 500 katika jimbo la Kasai katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kusababisha takriban watu 2,500 kuyahama makazi yao, anadolu inaripoti.

Mvua iliyonyesha kwa siku tatu iliharibu nyumba katika vijiji vya Kambamba na Bulape, alisema Pius Mapingo, afisa usalama wa Kasai.

“Mvua kubwa iliyonyesha iliezua paa za nyumba katika vijiji vya Kambamba na Bulape. Watu sasa wanaishi wazi na kuna hali ya kibinadamu. Kuna angalau nyumba 530 zilizoharibiwa, na kuwaacha takriban wakazi 2,500 bila makao,” rais wa shirika lisilo la kiserikali la Small Donation to Humanity, Marie-Claire Mutanda, alisema katika mahojiano na vyombo vya habari.

Mutanda aliitaka serikali kuwasaidia watu walioathirika.

AA