Mtanzania ametekwa nyara tarehe 4 ametekwa nyara na watu wasiojulikana nchini Nigeria. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Kigomba, Joseph Mlola, mseminari huyo alikamatwa Agosti 4 | Picha: Getty

Taarifa za kutekwa kwa Mahinini ambaye ni Frateri wa shirika la wamisionari wa Afrika (White Fathers) zimethibitishwa jana tarehe 7 Agosti na balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Benson Alfred Bana.

Mzaliwa wa Kabanga mkoani Kigoma Mahinini, alitekwa katika jimbo la Minna nchini Nigeria akiwa pamoja na raia wa Burkina Faso ambaye ni Padri aliyetambulika kwa jina la Paul Sanogo.

Milioni 31 zatakiwa ili waachiwe huru

Watekaji nyara wamedai kitita cha Naira milioni 100 sawa na shilingi milioni 31 ($12,000) za kitanzania.

Balozi Bana wakati anatoa taarifa kwa vyombo vya habari vya Tanzania amesema, ''Tukio la kutekwa ni kweli limetokea tangu Agosti 3 mwaka huu, sisi tunaokaa huku hatushangai, ni uhalifu ambao sio mgeni umeshazoeleka hapa Nigeria''. ''Wakishamteka mtu watekaji wanatangaza wanataka kiasi fulani, na hawa walipowateka hawa walitangaza wanataka Naira mılioni 100'' Bana aliongeza.

Kwa mujibu wa taarifa ya Balozi Bana imefahamika kwamba watekaji nyara huteka watu kwa sababu ya kujipatia fedha. Uwepo wa visa vingi vya utekaji nyara nchini Nigeria huenda madhara yakatokea kwa waliotekwa ili kuonesha mkazo wa watekaji kutaka fedha.

Bana amehakikisha kwamba shirika la kidini ambalo Mhanini anafanyia kazi linatambuliwa na jukumu la ubalozi ni kufuatilia kwa ukaribu tukio hili mpaka aachiwe huru.

TRT Afrika