Mtanzania ashinda mashindano ya uvumbuzi wa teknolojia Afrika

Mtanzania ashinda mashindano ya uvumbuzi wa teknolojia Afrika

Mashindano hayo yalihusisha vinara wa biashara na wavumbuzi kutoka Afrika.
  Mshindi wa medali ya uvumbuzi kwenye tekinolojia kwa vijana walio chini ya miaka 40   

Kutana na Deogratius Mosha raia wa Watanzania mwenye umri wa miaka 34 mmiliki wa kampuni ya Mainstream media ambaye amejikita katika maswala ya tekinolojia na uvumbuzi.

Deogratius ameunda tekinolojia ambayo inawawezesha wanafunzi waliokuwa kwenye vyuo vukuu nchini Tanzania kupata nyenzo za kujisomea kwa kutumia simu za mkononi bila gharama yoote

Ametatua tatizo ambalo liliwakabili wanafunzi wengi waliohitaji kutumia pesa ya kitanzania takriban elfu 40 mpaka 50 ili kuchapisha nyenzo za masomo.

Kwa kutumia tekinolojia hiyo Deogratius amechukua nyenzo zote zinazo tolewa na walimu katika kila chuo na kuzichapisha katika mfumo wa kidijitali kisha mwanafunzi yoyote anayehitaji kupata anajisajili bure na kupata taarifa zote bure.

Lakini pia teknolijia hiyo aliyovumbua inamruhusu kiongozi wa darasa katika kila chuo kupakia mtandaoni nyenzo zilizotolewa na mwalimu kisha kila aliyejiunga na mfumo anakuwa na uwezo wa kuzitumia.

Deo anasema mwaka jana mashindano haya yalitangazwa kwa lengo lakutafuta suluhisho la matatizo yanayo kabili nchi za afrika na watu wanaotambua kazi yake walimpendekeza kwenye tunzo hizo

Alikua akiwania nafasi hiyo pekeake kutoka Tanzania akishindana na watu wengine kutoka nchi mbali mbali na mwishoni baada ya mchakato kukamilika Deogratias akaibuka mshindi.

Kwa ushindi huo amepata utambuzi kwa kukamata medali ya uvumbuzi kwenye tekinolojia kwa vijana walio chini ya miaka 40 yaani "Forty under 40 Awards.’

TRT Afrika