Maelfu ya waombolezaji wakiwemo familia wamekusanyika katika shule ya seokondari ya Sinon jijini Arusha kuaga miili tisa ya watu waliofariki katika ajali ya kusombwa na maji kaskazini mwa Tanzania.
Miongoni mwa waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea tarehe 12 Aprili ni wanafunzi saba wa shule ya msingi ya Ghati katika eneo la Engosengiu Jijini Arusha Kaskazini mwa Tanzania.
Mtu mmoja anayeaminiwa alikuwa akijaribu kuwaokoa watoto wa shule hiyo pia alizama na kufariki katika dampo hiyo.
Taarifa za awali zilisema kuwa basi hilo lilikuwa limebeba wanafunzi kumi na moja, walimu wawili na dereva.
Mashahidi wanasema kuwa dereva wa basi hilo la shule alikuwa ametahadharishwa kutovuka eneo hilo bila kusikia.
Watoto wanne waliokuwepo ndani ya basi hilo pamoja na walimu wawili waliweza kuokolewa.
Mvua kubwa inaendelea kunyesha sehemu nyingi Tanzania ambapo umesababisha mafuriko na kuvunjika kwa baadhi ya barabara na madaraja kushindwa kuvukika.