Mfanyakazi mwenzake wa karibu aliliambia shirika la habari la AFP kwamba Nguema alikuwa karibu sana na rais Marehemu wa Gabon, Omar Bongo, akimhudumia kuanzia 2005 hadi kifo chake katika hospitali ya Barcelona.
Lakini mnamo mwaka wa 2009, rais aliyeondolewa, Ali Bongo, pindi tu alipochukua hatamu ya uongozi kwa kuchaguliwa kumrithi baba yake, alimuondoa Nguema na kumweka kando huku Nguema akianza muda wa miaka 10 kama mjumbe wa kijeshi katika balozi za Gabon nchini Morocco na Senegal.
Jenerali Brice Oligui Nguema, kiongozi mpya mteule wa Gabon kufuatia mapinduzi, alimtumikia kwa uaminifu kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo ya Afrika ya kati Omar Bongo kabla ya baadae kumng'oa mwanae, Ali Bongo, katika mapinduzi ya kijeshi Jumatano.
Nguema hakuonekana wakati taarifa za kwanza zilipokuwa zikisomwa na maafisa wakuu wa jeshi kwenye televisheni ya taifa kutangaza mapinduzi hayo.
Viongozi wa mapinduzi ya Gabon walifikia hatua ya kumteua baada ya kumuangusha Rais Ali Bongo Ondimba kufuatia uchaguzi wenye tashwishi wa Jumamosi ambapo mgombea huyo alitangazwa kushinda muhula wa tatu kwa asilimia 64.27 ya kura.
Nguema ni nani?
Nguema, mwenye umri wa miaka 48, anatokea kabila kuu la Gabon, Fang. Mara nyingi alilelewa na mamake katika jimbo la Haut-Ogooue, ngome ya Bongo.
Jenerali huyo alishikilia nyadhifa zake kama mlinzi wa baba yake kiongozi aliyeondolewa madarakani Omar Bongo, ambaye alitawala Gabon kwa mkono wa chuma kwa takriban miaka 42 hadi kifo chake mwaka 2009.
Nguema alijitokeza kama kiongozi wa hivi punde zaidi wa kijeshi barani Afrika huku kukiwa na sherehe za shangwe katika mitaa ya mji mkuu Libreville na kitovu cha kiuchumi cha Port-Gentil huku Bongo akiwa amefungwa kifungo cha nyumbani.
"Ni mtu anayefahamu vyema vyombo vya kijeshi vya Gabon, mwanajeshi mzuri, aliyefunzwa katika shule nzuri za kijeshi" ikiwa ni pamoja na chuo cha kijeshi cha Morocco cha Meknes, mwanachama wa Bongo Democratic Party (PDG) alisema kwa sharti la kutotajwa jina.
Mfanyakazi mwenzake wa karibu aliliambia shirika la habari la AFP kwamba Nguema alikuwa karibu sana na rais Marehemu wa Gabon, Omar Bongo, akimhudumia kuanzia 2005 hadi kifo chake katika hospitali ya Barcelona nchini uhispania.
Nguema alipata tena umaarufu mnamo 2018 kama mkuu wa ujasusi wa walinzi wa jamhuri, akichukua nafasi ya kaka wa kambo wa Ali Bongo Frederic Bongo, kabla ya kupandishwa cheo hadi jenerali miezi sita baadae.
Jenerali huyo aliyejengeka kiriadha amekuwa mkuu wa walinzi wa jamhuri, kikosi chenye nguvu zaidi cha jeshi nchini humo, tangu mwaka wa 2019, huku vyanzo vya karibu vikimuelezea kama mtu mwenye mvuto na anayeheshimika.