Kaimu mkuu wa polisi nchini Kenya Douglas Kanja amewahamisha maafisa wote wa kituo cha Kuare kiliko mita chache kutoka machimbo ya mawe ambako maiti zi;likutwa zimetupwa, ili kuruhusu uchunguzi huru kufanyika.
"Ili kuhakikisha uchunguzi wa haki na usio na upendeleo, nimewahamisha maafisa hao kutoka Kituo cha Polisi cha Kware," Kanja alisema katika mkutanoi na waandishi wa habari jijini Nairobi.
Kanja alisema kuwa wameopoa maiti nane kwa jumla na maiti zote ni za wanawake.
Kaimu huyo wa polisi pia alisema kuwa amewaagiza maafisa wanaoendesha uchunguzi kukamilisha ndani ya siku 21 ili matokea yawekwe wazi kwa umma juu ya waliohusika na mauaji hayo.
Inspekta Kanja pia amedokeza kuwa kwa mtazamo wake, huenda mauaji hayo yalihusiana na dini au ushirikina.
''Kwa kutumia rasilimali zetu za idara, maafisa wetu kwa ushirikiano na ofisi ya mwendesha mashtaka ODPP, wanafanya kazi bila kuchoka ili kukamilisha uchunguzi ndani ya siku 21,'' alisema Kanja.
Polisi bado wanaendelea na utafutaji wa maiti zingine ndani ya machimbo hayo.
Wakati huo huo, Mkuu wa kitengo cha ujasusi Mohammed Amin amewahakikishia Wakenya kuwa maafisa bora zaidi wametumwa kuendesha oparesheni na kuwaomba waruhusu uchunguzi ufanywe kikamilifu.
Amin amedokeza kuwa kuna mfanano kwa namna mauaji hayo yalifanyika na namna maiti zilitupwa.
''Utagundua kuwa modus operandi ilikuwa karibu sawa. Na ukiangalia umri kati ya 18 hadi 30 ukiangalia jinsia hawa wote ni wa kike,'' alisema Nurdin. ''Ukiangalia jinsi miili hiyo imekatwa vipande vipande na kufungwa, ni sawa. Ukiangalia mahali ambapo miili ilitupwa kwenye jalala, sehemu moja tu,” Amin alisema.
Hii alisema inatoa uwezekano kuwa huenda kulikuwa na kundi au watu waliohusiana waliotumia ushirikina au uhalifu wa kimatibabu.
“Kwa hiyo tunaangalia nini hasa? Je, tunashughulika na imani za kshirikina na kihalifu? Je, tunashughulika na wauaji mazoea, ambao pia wanahusishwa na shughuli za uhalifu? Tunaweza hata kushughulika na wahudumu wa afya wahuni ambao wanashughulika na shughuli za uhalifu,'' alionmgeza Amin.
Kiongozi huyo wa idara ya upelelezi aliwaomba wananchi kuwa na subira wakati uchunguzi uanendelea akilalamika kuwa maafisa wake walikabiliwa na umati uliokuwa na ghadhabu na kuwazuia kufikia eneo la ushahidi kuendesha uchunguzi wao.
mauaji haya yamekuj awakati taharuki imetanmda kutokana na madai ya watu kutekwa na watu wasiojulikana ambapo yamehusishwa na kuwaadhibu watu waliohusika na maandamano ya wiki mbili ya kupinga utawala wa Rais Ruto.
Polisi wamekanusha kuwa walihusika na utekaji wa aina yoyote.