Rais William Ruto alitangaza jioni ya 18 Aprili 2024 kuwa ajali ya helikopta ilikuwa imewauwa maafisa wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya, akiwemo mkuu wa jeshi Jenerali Francis Ogolla.
Rais Ruto ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa, kuanzia Ijumaa, Aprili 19, kwa heshima ya Jenerali Ogolla na wengine tisa walioangamia kwenye ajali hiyo.
"Huu ni wakati wa huzuni kubwa kwangu, kama Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya, udugu wa Jeshi la Ulinzi la Kenya na taifa kwa ujumla. Nchi yetu ya mama imepoteza mmoja wa majenerali wake shupavu, maofisa shupavu, askari na askari. wanawake," Rais Ruto alisema katiak hotuba kwa taifa Alhamisi.
Rais alisema pamoja na Jenerali Ogolla katika ajali hiyo kulikuwepo wanajeshi wengine 11, tisa ambao pia walifariki huku wawili wakinusurika.
Maafisa wengine waliofariki katika ajali hiyo ni Brigedia Swale Saidi, Kanali Duncan Keittany, Luteni Kanali David Sawe, Meja George Benson Magondu, Kapteni Sora Mohamed, Kapteni Hillary Litali, Sajenti Mwandamizi John Kinyua Mureithi, Sajenti Cliphonce Omondi, na Sajenti Rose Nyawira.
Waliuawa wakati helikopta yao ya kijeshi ilipoanguka muda mfupi baada ya kupaa.
Ndege hiyo, iliyokuwa katika ziara ya kuwatembelea wanajeshi waliotumwa kaskazini-magharibi mwa Kenya kukabiliana na wizi wa mifugo uliokithirin na inaropotiwa ilianguka dakika chache baada ya kuondoka katika Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Cheptuel iliyoko Kaunti ya Pokot Magharibi, Ruto alisema.
Askari wawili walinusurika katika ajali hiyo na wako hospitalini. Rais alisema, kuwa timu ya uchunguzi wa anga ilitumwa kutafuta chanzo cha ajali.
Katika kipindi hiki bendera zitapepea nusu mlingoti, mkuu wa nchi alisema.
Miili ya wanajeshi hao ililetwa usiku wa Alhamisi jijini Nairobi.