Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu (kushoto) akipongezwa na Rais wa China Xi Jinping baada ya kuzungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) mjini Beijing. /Picha: AFP

Rais Xi Jinping wa China alituma awakaribisha viongozi 50 wa Afrika wanaotembelea Beijing wiki hii kwa mkutano wa kilele uliokusudiwa kuimarisha uhusiano na bara ambalo wapinzani wa Magharibi pia wanalimezea mate.

Nchi mwenyeji iliwakaribisha kwa shngwe katika mkutano wa kilele wa Kongamano la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kama ishara ya heshima kwa washirika muhimu wa kibiashara.

China ni mshirika mkuu wa kibiashara barani Afrika na mkopeshaji mkubwa zaidi barani humo. Mifumo ya ukopeshaji imeifanya kumwaga mabilioni ya dola kwa ajili ya mikopo ya ufadhili wa miundombinu kupitia Mpango wake wa ''Belt and Road Initiative (BRI)''.

Viongozi wa Afrika walifika katika mkutano wa kilele mjini Beijing wiki hii wakiwa na matarajio makubwa ya biashara yenye uwiano bora na uwekezaji wa kutengeneza nafasi za kazi.

"Kati ya mikutano minane iliyopita nadhani hii ndiyo iliyofanikiwa zaidi kulingana na nguvu iliyoonyeshwa na Waafrika. Wanajua hasa wanachotaka. Wanatekeleza wakala wao kwa kufuata maslahi yao ya msingi,” David Monyae, mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo ya Afrika-China katika Chuo Kikuu cha Johannesburg, anaiambia TRT Afrika anapohudhuria mkutano huo.

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC) Moussa Faki Mahamat katika hafla ya sherehe ya Kongomano la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) mjini Beijing.

Rais Xi ameahidi zaidi ya dola bilioni 50 wa ufadhili Afrika katika kipindi cha miaka mitatu ijayo ili kutoa nafasi za kazi milioni moja, licha ya shutuma za diplomasia ya madeni na wimbi la nchi za Afrika kuhangaika kulipa madeni.

“Kinadharia, faida za muda mrefu za miradi hii ni kubwa kuliko madeni kwa sababu hurahisisha ukuaji wa uchumi. Hata hivyo, kipimo cha faida hizi kimekuwa kigumu kutathminiwa kwa sababu shinikizo la kufikia ulipaji husababisha dhana kuwa ni mzigo mzito kuliko faida,” anasema Beverly Ochieng, mchambuzi mkuu wa Control Risks, kampuni ya ushauri katika Afrika Magharibi.

"Nchi za Kiafrika pia zinapendelea sera ya China ya kutoingilia mambo yao ya ndani pamoja na masharti mepesi (ya mikopo)," anaongeza.

Mwelekeo mpya

Mkutano huo unatarajiwa kutoa mwelekeo kuhusu ushirikiano wa China na Afrika ya baada ya Covid-19. Rais Xi ameashiria kupinguza kwa miradi ya miundombinu isiyo na faiga na kuzingatia zaidi biashara na mikopo kupitia taasisi za kifedha, kulingana na Ochieng.

"China imerekebisha uwekezaji wake kwa njia endelevu zaidi ya kukopesha kutokana na mzozo wake wa kiuchumi nyumbani. Pia imejadiliana upya masharti ya mikopo na nchi kama Zambia na Kenya ili kuendeleza uhusiano na kuhakikisha madeni yanalipwa," Ochieng anasema.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akielekea kwenye jukwaa kutoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa tisa wa Wakuu wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).

Kuelekea katika mkutano huo, viongozi wa Afrika walitafuta mikopo zaidi kwa ajili ya miradi mikubwa ya mabomba ya mafuta, usambazaji wa umeme na njia za reli, kulingana na taarifa zilizotolewa kufuatia mikutano ya moja kwa moja na mwenyeji wao Xi.

Nigeria ilitia saini makubaliano ya nishati ya nyuklia. Salva Kiir wa Sudan Kusini alijadiliana na kampuni ya China mipango ya kujenga bomba mbadala la mafuta kupitia Ethiopia na Djibouti ili kuimarisha mauzo ya nje.

Tanzania na Zambia zilitia saini makubaliano ya awali ya mradi wa reli wa njia muhimu ya mauzo ya shaba kutoka eneo la Copperbelt nchini Zambia.

Nishati mbadala na hali ya hewa - ambapo China inatazamia kuwa kiongozi wa kimataifa - pia ni mada za kuzungumziwa katika mkutano huo.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa aliambia makampuni ya China kwamba anatafuta uwekezaji katika sekta ya nishati wakati nchi yake ikikabiliana na tatizo la umeme nchini humo, mbaya zaidi kuwahi kutokea katika miongo kadhaa ambayo imeharibu biashara na maisha.

"China ina rekodi ya kuthibitishwa katika kuendeleza ufumbuzi wa ubunifu wa nishati mbadala. Kwa pamoja, tunaweza kuunda ufumbuzi wa nishati endelevu na rafiki wa mazingira ambao unanufaisha nchi zetu zote mbili," Ramaphosa aliambia kongamano la biashara mjini Beijing.

Wajumbe kutoka Burkina Faso wakijiandaa kuingia katika ukumbi mkuu kabla ya ufunguzi wa Kongamano la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) unaoendelea mjini Beijing.

Misuli ya mataifa kama ya China barani Afrika katika miongo miwili iliyopita imebadilisha jinsi bara hilo linavyoamiliana na mataifa ya Magharibi.

Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen, alisema kwa mzaha kuwa haina maana kwa Umoja wa Ulaya kujenga barabara kati ya mgodi wa shaba na bandari ikiwa zote mbili zinamilikiwa na China.

Kupiganiwa kwa Afrika

Wachambuzi wanaonya, hata hivyo, kwamba ushawishi unaokua wa Beijing sio hasara kwa Afrika haswa katika uhusiano wa kidiplomasia na mataifa mengine yanayoangalia hisa katika mahitaji ya uwekezaji ya bara hilo.

Wanasema wahusika wengine bado wanaweza kufanya kazi katika maeneo sawa na Uchina lakini kwamba nchi za Afrika lazima zijitahidi kujiletea maendeleo yao badala ya kushikamana na upande wowote katika vita vya ubabe vya kimataifa.

"Suala letu kama Waafrika sio kuegemea upande wowote, tunahitaji kuwa na nia inayounga mkono Afrika na fanya uhusiano na mtu yeyote ambaye anatuletea faida na faida," Monyae anasema.

Mataifa yenye nguvu duniani yataendelea kutafuta ushawishi kupitia diplomasia ya mkutano huo ili kupata marafiki na kuungana na Afrika.

Mikutano hiyo imechukua umuhimu mkubwa zaidi huku kukiwa na hali ya mvutano wa kisiasa wa kijiografia uliozidishwa na vita vya Urusi na Ukraine.

"Nchi za Kiafrika zitaendelea kuwa sehemu ya mashindano ya kijiografia. Bara bado linaonyesha fursa ya maendeleo ya kiuchumi na raslimali watu,” Ochieng anasema.

"Kumekuwa na ushindani mkubwa na mataifa mengine yenye nguvu duniani kwa ajili ya mikutano kama hiyo ambayo itaongeza uwepo wao katika bara," anaongeza.

TRT Afrika