Misri yakanusha kujiondoa katika kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israeli huko ICJ

Misri yakanusha kujiondoa katika kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israeli huko ICJ

Cairo "imedhamiria kuchukua hatua zinazohitajika kulaani matendo ya Israeli", amesema ofisa mmoja.
Afrika Kusini inatafuta hatua mpya za dharura kutoka ICJ kuhusu mashambulizi ya Israeli dhidi ya Rafah. Picha / Reuters/AA 

Misri ilikanusha siku ya Jumamosi madai ya kubatilisha ushiriki wake katika kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel, iliyowasilishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuhusu madai ya "mauaji ya kimbari" huko Palestina.

Idhaa ya kibinafsi ya Al Qahera News ilinukuu chanzo ambacho hakikutajwa jina kikisema kwamba "taarifa zinazosambazwa na vyombo vya habari vya Israeli kuhusu Misri kujiondoa kuunga mkono kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israeli katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki hazina msingi."

Chanzo hicho kimesisitiza kuwa "Misri imejidhatiti kuchukua hatua stahiki za kuilaani Israeli katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki," bila kutoa taarifa zaidi kuhusu namna ya hatua hizo.

Wiki iliyopita, Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri ilitangaza nia yake rasmi ya kuingilia kati na kuunga mkono kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israeli katika Mahakama ya ICJ.

Azimio la Umoja wa Mataifa

Wizara hiyo ilifafanua kuwa uamuzi wake ulichochewa na kuongezeka kwa kiwango cha mashambulizi ya Israel dhidi ya raia wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.

Israeli iliendelea na mashambulizi yake ya kikatili kwenye Ukanda wa Gaza licha ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutaka kusitishwa mara moja mapigano katika eneo hilo.

Takriban Wapalestina 35,400 wameuawa tangu wakati huo, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na karibu wengine 79,400 kujeruhiwa tangu Oktoba mwaka jana kufuatia shambulio la Hamas.

Israeli inashutumiwa kwa "mauaji ya halaiki" katika mahakama ya ICJ, ambayo imeiamuru Tel Aviv kuhakikisha vikosi vyake havifanyi mauaji ya halaiki na kuchukua hatua za kuhakikisha kwamba msaada wa kibinadamu unatolewa kwa raia huko Gaza.

TRT Afrika