Walaghai wamewasilian na nchi za ulaya wakidai wanawakilisha mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat / Picha: AFP

Tume ya Umoja wa Afrika inasema mifumo yake ya mawasiliano imedukuliwa na walaghai ambao walifanya mawasiliano na nchi tofauti wakijidai kuwa viongozi wa tume hiyo.

" Walaghai walipiga simu za video za uwongo kwa viongozi wa nchi kadhaa za Ulaya wakidai kuwa ni mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika Moussa Mahamat," msemaji wa mwenyekiti wa Tume hiyo Ebba Kalondo ameelezea.

Taarifa ambayo Tume hiyo imetoa yaashiria kuwa barua pepe ghushi ilitumika kufanya mawasiliano na nchi za ulaya, zikidai kuwa mawasiliano kutoka kwa naibu mkuu wa wafanyakazi wa Tume hiyo kwa niaba ya ofisi ya mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika.

" Umoja wa Afrika unasisitiza uzingatiaji wake madhubuti wa itifaki ya kidiplomasia na matumizi ya kipekee ya mawasiliano aina ya "Note Verbale" kwa maombi ya ushirikiano wa hali ya juu," ameongezea.

TRT Afrika