Sehemu ya michoro kwenye mitaa ya Nairobi yenye kuiunga mkono Palestina. Picha: AA  

Mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza yamefikia mwezi wa tano yakiwa yameua watu 31,341na kujeruhi watu 73,134.

KIkundi cha wakenya kikiwaunga mkono wapalestina mbele ya michoro hiyo./Picha: AA

Kulingana na wasanii hao, michoro hiyo inawakilisha upinzani wa wapalestina dhidi ya mashambulizi kutoka Israel, katika eneo la Gaza.

Michoro hiyo inapatikana katika mitaa ya Nairobi.Picha: AA

Utamaduni wa sanaa za mitaani ni zenye kuhamasisha sana katika mji mkuu wa Kenya, ukiwa na michoro mbalimbali ya rangi na michoro kwenye kuta za majengo ya jiji, madaraja na vitongoji.

Michoro hiyo huonesha mshikamano kwa watu wa Palestina wanaopitia madhila ya mashambulizi kutoka kwa majeshi ya Israel. Picha: AA

Wasanii hao hutafuta dhima mbalimbali kupitia masuala ya kijamii na kisiasa yanayoathiri maisha ya watu.

TRT Afrika