Mchungaji huyo ametiwa nguvuni anasaidia polisi katika uchunguzi / Picha : reuters 

Polisi katika eneo la Webuye Magharibi mwa Kenya wanamshikilia mshukiwa aliyekutwa na vipande vya mwili wa binadamu ndani ya buti ya gari lake.

Katika taarifa kwenye ukurasa wake wa X, Ofisi ya mwendesha mashtaka DCI ilisema kuwa mwanamume mmoja amekamatwa akiwa na vipande vya mwili vilivyochomeka ndani ya box iliyofichwa kwenye buti ya gari lake.

''Polisi huko Webuye wanamshikilia kwa uchunguzi mtu anayejiita kasisi ambaye ndani ya gari lake kulikutwa sehemu za binadamu zikiwa zimefichwa kwenye , baada ya kuipeleka kwenye eneo la kuosha magari,'' ilisema taarifa hiyo.

Mshukiwa huyo alijitambulisha kama mchungaji wa kanisa na amezuiliwa akiwasaidia polisi katika uchunguzi wao.

Mhudumu wa kuosha gari alipata mshtuko alipofungua buti na kuona mguu wa binadamu ukichomoza, na baada ya kupekua zaidi polisa wanasema alikuta vipande zaidi vya zaidi vya mwili wa binadamu.

Meneja wa kituo hicho aliwaita polisi na ndipo wakamkamata mshukiwa.

Hii inakuja wakati bado kuna shauku juu ya mauaji yaliyofanyika katika kanisa la Shakahola, mjini Malindi, Pwani ya Kenya, ambapo makaburi ya watu wengi yaligunduliwa.

Uchunguzi ulionesha kuwa wengi wao walikufa kutokana na kunyimwa kula na kunywa kwa imani kuwa wanafunga ili wakutane na Mungu wao.

Mamia ya waumini wengine walinusuriwa wakiwa wamedhoofika kutokana na njaa. Mshukiwa Paul Mackenzie, ambaye alikuwa mchungaji wa kanisa hilo, alikamatwa na kufunguliwa mashtaka.

Kesi yake imeanza kusikilizwa katika mahakama ya Mombasa, pwani ya Kenya.

TRT Afrika