Na Coletta Wanjohi
Istanbul, Uturuki
Uchunguzi unaendelea nchini Kenya wa mauaji ya watu ambao miili yao imepatikana katika dampo la Embakasi jijini Nairobi.
Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa, miili yote ilikuwa ya wanawake. Mpaka sasa, polisi inasema imemkamata mshukiwa mkuu wa mauaji hayo.
Collins Jomaisi Khalusha mpaka sasa, kwa mujibu wa polis ndie mshukiwa mkuu anaedaiwa kuua wanawake 42 kati ya mwaka 2022 na 11 Julai 2024.
Kwa mujibu wa polisi, Collins alikiri kuwa muathirika wake wa kwanza alikuwa mke wake. Miili iliyotolewa katika machimbo ilikuwa katika hali mbya, mengine ikiwa imekatwa katwa, na kufungua katika karatasi za plastiki ndani ya magunia na kutupwa.
Polisi inasema kuwa kufikia Jumatatu, miili 9 ilikuwa tayari imepatikana, tofauti na aliyeitoa miilini hiyo ambae anasema ilikuwa 13.
Hii sio mara ya kwanza kwa mauaji ya aina hii kutokea nchini Kenya.
Itakumbukwa kwamba, mwaka 2008 mtu mmoja kwa jina la Geoffrey Matheri mwenye umri 26, alikamatwa na polisi na wanawake wawili wakaokolewa katika mji wa Naivasha wakiwa katika hali mbaya na hata kushindwa kuongea.
Matheri alikiri kuwa alikuwa akiwateka nyara wanawake, kuwaua na kunywa damu yao. Matheri alidai kuwa alishawishiwa na mkuu wake wa kanisa kuua na kumletea sehemu za mwili. Mwaka 2010, Philip Onyancha akiwa na umri wa miaka 32, alikamatwa baada ya yeye nae kukiri kuwaua watu 17, haswa wanawake.
Yeye alidai kuwa aliingizwa kwenye ibada na mwalimu wake akiwa bado mwanafunzi, ambaye anadai aliambiwa aue watu 100 na anywe damu yao ili ashafishe nyote
Bila kusita, Onyancha aliwaongoza polisi katika maeneo ambayo alikuwa ametupa miili kadhaa. Mwaka 2016 katika mji wa Nakuru, mwendesha piki piki aina ya Tuktuk alikamatwa alipopatikana akisafirisha mwili ya mwanamke.
Wanawake 10 walikuwa wameuawa ndani ya miezi sita, waliolengwa zaidi walikuwa madada poa. Macho, ngozi ya uso na sehemu zao za siri zilinyofolewa.Mauaji haya yaliibua hasira za wananchi.
Januari mwaka huu nchini kote kulishuhudiwa maandamano ya kupinga mauaji ya wanawake nchini humo.
Takwimu zilionyesha takriban wanawake 500 waliuawa katika vitendo vya mauaji ya wanawake kuanzia Januari 2016 hadi Desemba 2023.Haya ni baadhi tu ya visa vya wauaji sugu katika historia ya Kenya.
Takwimu zilionyesha takriban wanawake 500 waliuawa katika vitendo vya mauaji ya wanawake kuanzia Januari 2016 hadi Desemba 2023.
Haya ni baadhi tu ya visa vya wauaji sugu katika historia ya Kenya.Wataalam wa afya wanasema hakuna mtu ambaye anaweza kuitwa tu muuaji sugu, ni tabia ambayo inajikuza kwa sababu tofauti.
Wanadai ni vigumu kujua kwa nini watu huamua kufanya mauaji kama haya yanayolenga jinsia moja au kwa njia moja.
Huku wengine huenda wakawa na shida za kiakili, matumizi ya dawa ya kulevya na ushawishi kutoka kwa watu kunaweza kuchangia tabia hii.
Wengine inadaiwa hubadilika kuwa wauaji sugu kutokana na changamoto za kiakili zinazohusishwa na malezi yao. Kumekuwa pia na taswira ya ushawishi potovu wa kidini kuhusishwa katika mauaji tuliyotaja.
Katika kisa ambacho kimeikumba nchi kwa sasa ya miili ya wanawake kupatikana imetupwa katika eneo la machimbo, Hivi sasa hali ya taharuki imetanda huku wananchi wakitaka majibu, ni nani hasa alihusika katika mauaji hayo na kwa nini?