Kilimo ni moja wapo ya sekta muhimu inayochochea ukuaji wa uchumi katika nchi nyingi za Kiafrika ikiwa ni pamoja na Nigeria   Photo : Reuters

Na Jakkie Cilliers

Tunapolinganisha historia na matarajio ya Afrika baada ya uhuru na wastani katika maeneo mengine, ni wazi kuwa bara hilo kwa ujumla linarudi nyuma katika hatua muhimu za maendeleo, kama inavyoonyeshwa kwenye chati ya wastani wa pato la taifa kwa kila mwananchi.

Chati inaonyesha data hadi mwaka 2021, na inajumuisha utabiri wa 2043, huku athari ya 2020/2021 ya Uviko -19 ikionekana haswa.

Mambo yanaimarika barani Afrika lakini polepole kuliko kwingineko.

Baadhi ya nchi, mara nyingi ndogo, zinakua kwa kasi. Bado, nchi nyingi zinatatizika kwa sababu nyingi za ndani . Lakini pia vita vya Ukraine vinazuia uwezo wa Afrika.

Kuna kila sababu ya kuwa na wasiwasi kuhusu athari za kisiasa na nyinginezo za pengo hili linaloongezeka. Hata hivyo, kuna baadhi ya mambo yanayohusiana na ukuaji wa binadamu kama vile umri wa kuishi na vifo vya watoto wachanga.

Kuongezeka kwa pato la kiuchumi

Mwenendo wa sasa katika maeneo kadhaa - kutoka kwa utawala bora na mgawanyiko wa idadi ya watu hadi mapinduzi ya kilimo na utekelezaji kamili wa Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika - unatoa picha ya uwezekano wa maendeleo wa Afrika katika hali bora zaidi ya dunia.

Mwaka 2022, pato la taifa kwa kila mwananchi barani Afrika lilikadiriwa kuwa dola za Marekani 4,955.

Kufiuatia mtindo wa maendelo barani Afrika hii ingefikia dola za Marekani 7,157 mwaka 2043 , kama vile matarajio ya Ajenda ya muda mrefu ya Umoja wa Afrika ya mwaka 2063.

Katika hali ya pamoja pato la taifa kwa kila mtu linaweza kuwa 54%. Badala ya uchumi wa Afrika wa dola trilioni 3.2 mwaka 2022 ambao unaongezeka hadi dola trilioni 8.7 mwaka 2043, uchumi wa Afrika unaweza kufikia dola trilioni 15.2.

Hizi ni tofauti kubwa sana na zinaonyesha uwezo mkubwa wa maendeleo wa Afrika.

Sekta ya nguo ya Afrika Kusini inatoa ajira kwa wengi Photo : Reuters

Utabiri huu unachukulia kuwa kuna mazingira wezeshi ya kimataifa (yale tunayoita Ulimwengu Endelevu) ambayo huongeza uwezo wa maendeleo wa Afrika.

Kwa kuzingatia kuongezeka kwa mvutano kati ya nchi za magharibi na Uchina, uvamizi wa Urusi kwa Ukraine na maendeleo mengine, mradi hivi karibuni uliongeza mada ambayo iligundua athari za hali tofauti za ulimwengu kwa uwezo wa Afrika kupata maendeleo.

Mandhari ya Afrika katika ulimwengu inawasilisha na kutoa mifano ya matukio matatu ya ziada ya kimataifa: ulimwengu uliogawanyika, ulimwengu ulio katika vita na ulimwengu wa ukuaji.

Hali ya Ulimwengu kwenye vita ndiyo yenye athari mbaya zaidi kwa kila mtu, kwani faida ya jumla ni chini ya nyingine yoyote.

Hali ya ukuaji wa ulimwengu inaongoza kwa matokeo bora ya kiuchumi lakini kwa uharibifu wa usawa na juhudi za kudhibiti gesi chafu duniani, na kusababisha athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa.

Kufuatia warsha kadhaa, mwelekeo wa sasa wa kimataifa unaonekana kukadiria mwelekeo wa ulimwengu uliogawanyika.

Huu ni mustakabali wa ukandamizaji zaidi, utofauti mkubwa, na uwezekano wa mgawanyiko unaokua kati ya nchi tajiri za magharibi na zingine. Hali ya ukweli lazima itatofautiana.

Kinyang'anyiro kwa ajili ya Afrika

Ukubwa wa uchumi wa Afrika, pato la taifa kwa kila mtu, na viwango vya umaskini ni tofauti kabisa katika hali hizi nne.

Takwimu inayoambatana na hii inaonyesha ukubwa wa jumla ya uchumi wa Afrika katika mwaka 2019 na kisha kwa kila hali katika mwaka 2043. Inaonyesha faida katika ukuaji wa uchumi wa Afrika katika ulimwengu endelevu.

Licha ya idadi kubwa ya watu na nchi nyingi wanachama, Afrika ni mshiriki mdogo wa kimataifa.

Hadhi yake imeinuliwa, wakati mwingine, kutokana na ushindani wa nchi za mashariki-magharibi, jukumu lake katika kutoa nishati ya mafuta, wakati wa vita dhidi ya ugaidi, na kuzingatia maendeleo kwa kuunda malengo ya milenia na maendeleo endelevu.

Hivi karibuni, Afrika imekuwa eneo la ushindani kati ya nchi za magharibi, Uchina na Urusi na ushindani wa madini yanayowezesha mapinduzi ya nne ya viwanda kuzidi kushika kasi.

Hali ya Ulimwengu endelevu ingehitaji kukomesha mvutano kati ya Marekani na Uchina na mageuzi ya mfumo wa sheria wa kizazi kijacho unaoshughulikia Uchina, Marekani, Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Kusini inayokua duniani.

Mwelekeo wa sasa wa kuelekea ulimwengu uliogawanyika unazuia maendeleo ya Afrika.

Ikilinganishwa na Ulimwengu endelevu, ulimwengu uliogawanyika una kiwango cha juu zaidi cha uzalishaji wa kaboni duniani unaosababisha mabadiliko ya haraka ya hali ya hewa.

Barani Afrika, pato la taifa kwa kila mtu litakuwa chini kwa asili mia 17%, na umaskini uliokithiri utakuwa juu kwa asili mia 55% katika ulimwengu uliogawanyika ikilinganishwa na ulimwengu endelevu.

Hata hivyo, ni ushirikiano wa kina zaidi wa kiuchumi na kisiasa barani Afrika, ukisaidiwa na ukuaji wa haraka na endelevu wa uchumi unaoweza kufidia nafasi ndogo ya bara katika kuunda mwelekeo wa kimataifa.

Hii ikiashiria haja ya haraka ya kusonga mbele kwa kasi zaidi katika suala hili.

Mwandishi, Jakkie Cilliers, ni mkuu wa African Futures & Innovation katika ofisi ya Pretoria ya Taasisi ya Mafunzo ya Usalama. Kanusho: Maoni yaliyotolewa na mwandishi si lazima yanaashiria maoni na sera za uhariri za TRT Afrika.

TRT World