Katibu Mkuu wa Baraza la Wakimbizi la Norway (NRC) Jan Egeland alimtembelea  Anwar aliyekimbia Khartoum na kuwasili Port Sudan miezi minne iliyopita, ana ulemavu ulioathiri miguu yake/ Picha: NRC 

Vita vya mwaka mmoja na nusu vimesababisha idadi kubwa ya watu kuelekea kuporomoka kwa Sudan, huku zaidi ya watu milioni 20 wakikabiliwa na ghasia na njaa inayoongezeka na kulazimishwa kuyahama makazi yao, Katibu Mkuu wa Baraza la Wakimbizi la Norway (NRC) Jan Egeland alisema katika ziara nchini humo.

"Miaka 20 iliyopita, tulikuwa na marais na mawaziri wakuu walioshiriki kukomesha ukatili huko Darfur. Leo kuna maisha mengi zaidi hatarini - hii ndio shida mbaya zaidi ulimwenguni - lakini kuna changamoto ya ukimya kuihusu. Ni lazima tuuamshe ulimwengu kabla ya njaa kuikumba kizazi cha watoto hapa Sudan,” alisema Egeland.

Bakhita yuko yeye na binti yake huko Port Sudan. Binti yake amepooza, huku akiwa na changamoto nyengine za kiafya. / Picha kutoka Norwegian Refugee Council

Mashirika ya kibinadamu ya ndani na ya kimataifa bado yana changamoto za kufikisha chakula na mahitaji muhimu katika maeneo yote kwani vita vinaendelea.

"Nimejionea kwa macho yangu mwenyewe, huko Darfur na mashariki, matokeo mabaya ya mashambulizi ya kiholela na vita visivyo na maana. Mwezi uliopita pekee, zaidi ya watu 2,500 waliuawa na zaidi ya watu 250,000 wapya walihama makazi yao," ameongezea.

Takwimu zinaonyesha kuwa mzozo wa Sudan umelazimisha idadi kubwa ya watu kuhama makazi yao. Zaidi ya watu milioni 11 wamehamishwa nchini humo, na wengine milioni tatu wanatafuta hifadhi nchini Chad, Misri, Sudan Kusini na mataifa mengine jirani.

Kote Sudan, njaa kali inaripotiwa kuwauwa watu kila siku.

Takriban watu milioni 24—nusu ya idadi ya watu—wanahitaji chakula, ikiwa ni pamoja na milioni 1.5 walio katika makali ya njaa.

Maeneo ya mijini na vijiji vya mbali vimetahiriwa. Inasemekana kuwa zaidi katika maeneo kama mji mkuu wa Khartoum, ambao zamani ulikuwa ni kitovu cha uchumi wa nchi.

"Njaa inayoendelea hapa ni janga la mwanadamu," alisema Egeland. "Huko Darfur, nilikutana na wanawake ambao wamesalimika, wakila mlo mmoja wa majani yaliyochemshwa kwa siku. Pande zinazopigana, ambazo zinazuia ufikiaji wa jumuiya hizi, zinalaumiwa moja kwa moja kutokana na hilo. Mgogoro huu wa kibinadamu unaweza kukomeshwa wakati wowote."

TRT Afrika