Wanajeshi kadhaa wa Afrika Kusini wameuawa wakiwa katika ujumbe wa amani Afrika Kusini/ Picha: Reuters

Kikosi cha Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (SAMIDRC) kiko nchini DRC kusaidia serikali ya nchi hiyo kurejesha amani na usalama Mashariki mwa DRC.

Mnamo Mei 2023, SADC iliidhinisha SAMIDRC kuleta utulivu katika eneo hilo, na kuipa mamlaka ya kushiriki katika mapambano ya moja kwa moja na makundi yenye silaha.

Ililenga kuwa na wanajeshi 5,000 kutoka Malawi, Afrika Kusini na Tanzania, lakini ni wanajeshi 1,300 pekee ambao wamepelekwa huko kufikia sasa.

Eneo la Mashariki mwa DRC limeshuhudia ongezeko la migogoro na kukosekana utulivu unaosababishwa na kuibuka tena kwa vikundi vyenye silaha.

Afrika Kusini imesema ina nia ya kuleta amani DRC / picha : @SANDF_ZA

Hii ilikuwa baada ya DRC kukataa kikosi cha Afrika Mashariki kiendelee na oparesheni ya amani nchini humo , ikiilaumu kwa kuhusiana na kikundi chenye silaha cha M23.

Jeshi hilo limeundwa na wanajeshi kutoka Malawi, Afrika Kusini na Tanzania.

Linashirikiana na jeshi la DRC (FARDC), katika kupambana na makundi yenye silaha yanayofanya kazi Mashariki mwa DRC.

Kupelekwa kwa SAMIDRC ni kwa mujibu wa kanuni ya ulinzi wa pamoja na hatua za pamoja zilizoainishwa katika Mkataba wa Ulinzi wa Pamoja wa SADC (2003).

Mkataba huo unasisitiza kuwa;

"Shambulio lolote la silaha litakalofanywa dhidi ya moja ya Nchi Wanachama litachukuliwa kuwa tishio kwa amani na usalama wa kikanda na litakabiliwa na hatua za pamoja za haraka".

" Wanajeshi wetu 14 wameuawa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) baada ya kushambuliwa," Rais Cyril Ramaphosa alisema katika taarifa baada ya wanajeshi wa kikosi hicho kulaumiwa na M23.

Rais Lazarus Chakwera alisema Jumatano kwamba uamuzi wake ulikusudiwa "kuheshimu tamko la kusimamisha mapigano na pande zote", ingawa mapigano yanaendelea.

Katika taarifa yake iliyosomwa kwenye televisheni ya serikali Jumatano jioni, alisema kuondolewa kwa wanajeshi "kutafungua njia kwa mazungumzo yao yaliyopangwa kuelekea amani ya kudumu".

Afrika Kusini hata hivyo haijasema itaondoka DRC.

" Kuwepo kwa Afrika Kusini nchini DRC kunategemea ujumbe wa SAMIDRC, ambao una muda wa kufanya kazi na tarehe ya mwisho kufanya hivyo. Lengo hilo litaisha kwa mujibu wa utekelezaji wa hatua mbalimbali za kujenga imani na wakati wa usitishaji vita ambao tumetoa wito utakaposhika mizizi, " Rais Ramaphosa alisema.

Novemba 2024, mpango huo wa amani nchini DRC uliongezewa muda wa mwaka mmoja na viongozi wa nchi za Afrika Kusini.

Ikiwa sasa Malawi inajiondoa katika kikosi hiki haijulikani ikiwa nchi zingine zitaongeza wanajeshi.

TRT Afrika