Na Tooba Masood
Wizara ya afya ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ilitangaza siku ya Jumanne kwamba ugonjwa wa ajabu unaoathiri jimbo la Kwango kusini magharibi umetambuliwa kama malaria kali, kulingana na ripoti iliyotolewa na Reuters.
“Fumbo hilo hatimaye limefumbuliwa. Ni malaria kali inayokuja kwa njia ya ugonjwa wa kupumua... na kudhoofishwa na utapiamlo,” ilisema taarifa ya wizara ya afya.
Maafisa wa wizara walibaini kuwa utapiamlo ndio chanzo kikubwa cha magonjwa, huku maambukzi hayo sasa yakifikia 592 na kiwango cha vifo kufikia asilimia 6.2.
Mapema mwezi huu, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitahadharishwa kuhusu mlipuko wa ugonjwa ambao haujatambuliwa nchini DRC, ambao sasa umeripotiwa kusababisha vifo vya watu 143.
Kufuatia siku kadhaa za mkanganyiko kuhusu sababu ya ugonjwa huo, maafisa sasa wanaonyesha kuwa matokeo ya uchunguzi yanaonyesha kuwa ugonjwa wa Malaria unaweza kusababisha mlipuko huo mbaya katika jimbo la Kwango nchini DRC.
Wataalam, hata hivyo, wanaonya kuwa vimelea vingine vinaweza pia kuhusika.
Wiki iliyopita, kati ya sampuli 12 za awali zilizopimwa, 10 zilipatikana na malaria.
"Muda uliochukua kubaini ugonjwa huo kutoka mwisho wa Oktoba hadi sasa - kufikia uchunguzi huu unasisitiza hitaji muhimu la kuimarisha mifumo ya afya na kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya uhakika na vipimo vya haraka vya uchunguzi," Dk Krutika Kuppalli, mtaalam wa magonjwa ya kuambukiza katika Chuo Kikuu cha Texas ameaimbia TRT World.
"Bila uchunguzi wa wakati, matabibu wanakabiliwa na changamoto kubwa katika kuamua mipango ya matibabu yenye ufanisi zaidi kwa wagonjwa," aliongeza.
"Katika kesi hii, uwepo wa malaria unaonyesha umuhimu wa kugundua mapema - ambayo ingefanyika kama RDTs zingepatikana katika eneo hilo. Matibabu ya kupambana na malaria na huduma ya usaidizi ingeweza kubadilisha matokeo ya kliniki," Kuppalli alielezea.
"Zaidi ya hayo, ukali wa ugonjwa unaochochewa na utapiamlo mkali unasisitiza haja ya kushughulikia masuala ya msingi kama vile uhaba wa chakula ili kuboresha afya kwa watu walio na magonjwa ya kuambukiza," aliongeza.
Kulingana na Kuppali, hali hii hutumika kama ukumbusho kamili wa hitaji kubwa la kuimarisha ufuatiliaji, uchunguzi, na upatikanaji wa huduma.
Wakati malaria ndiyo inayolengwa wakati huu, milipuko ya siku zijazo inayohusisha magonjwa yanayoenea kwa kasi inaweza kuwa tishio kubwa zaidi kwa usalama wa afya duniani.