Eneo la mashariki mwa DRC limekumbwa na ghasia kwa miaka kadhaa sasa. / Picha: AFP

Mamia ya wanachama wa kundi linalojiita la kujilinda la jamii walijiwasilisha kwa jeshi la Congo siku ya Jumatatu na kutia saini "makubaliano ya amani" ya upande mmoja katika kaskazini mashariki mwa DRC, mwandishi wa habari wa AFP alisema.

Wakiwa wamevalia kiraia na bil akubeba silaha, kundi hilo la vijana lilifika katika kituo cha mkoa wa Bunia wakiwa na magari kadhaa na kutia sahihi mpango huo huku wenyeji wakiwa wamepigwa na butwaa.

Wakati msafara huo ukiingia jijini, maduka na biashara zilifungwa mara moja, mwandishi alisema.

Kundi hilo lilisema walikuwa wa shirika la ulinzi lililoanzishwa mwaka wa 2019 kutetea maslahi ya jamii tano ambazo zilikuwa "wahasiriwa wa ukatili katika jimbo la Ituri" karibu na mpaka na Uganda.

Ghasia za kikabila

Kundi hilo linalojulikana kama "Zaire", linasema linawakilisha jamii za Hema, Mambisa, Alur, Akongo-Nyali na Ndo-Okebu na ni mpinzani wa Codeco ("Cooperative for the Development of Congo"), kundi la wanamgambo lenya maelfu ya wanachama, wanaosema dhamira yao ni kulinda kabila la Lendu dhidi ya Wahema na washirika wao.

Baada ya miaka kumi ya utulivu, machafuko kati ya makabila yalianza tena mwishoni mwa 2017, na kusababisha vifo vya maelfu ya raia huku zaidi ya milioni moja wakikimbia.

Mzozo wa awali kati ya wanamgambo hasimu ulisababisha maelfu ya watu kuuawa kati ya 1999 na 2003 kabla ya kuingilia kati kwa kikosi cha kulinda amani cha Ulaya.

"Tuko hapa leo tumejitolea na tayari kujiunga na mchakato wa amani" na kushiriki katika mpango wa ushirikiano wa jamii utakaoongozwa na mamlaka ya Congo, msemaji wa kikundi Jean-Marie Ngadjole alisema.

Usafiri huru wa watu na bidhaa

Aliongeza kuwa kikundi hicho kimejitolea kuhakikisha usafirishaji huru wa watu na bidhaa zao katika jamii zote na akahimiza mamlaka "kuwezesha kuachiliwa kwa wanachama wake wote waliofungwa.

Jenerali Chalwe Muntutu Ngwashi, naibu gavana wa Ituri, alisema "alizingatia" kujitolea kwa kikundi hicho na akahimiza "kusameheana" na "maridhiano."

Lakini pia alihimiza "hebu pia tuondoe uhasama ndani ya mioyo yetu."

Hakuna tarehe iliyowekwa ya kupokonywa silaha kwa kundi hilo na kumekuwa na makubaliano sawa na makundi mengine, ikiwa ni pamoja na Codeco, ingawa athari kwa msingi imekuwa ndogo na vurugu kuendelea.

TRT Afrika