Mahakama Kuu Kenya yasema kifungo cha maisha ni kinyume na katiba

Mahakama Kuu Kenya yasema kifungo cha maisha ni kinyume na katiba

Jaji amesema ni lazima kifungo hiki kipewe miaka, miezi na masiku
Jaji wa Kenya ameamua kuwa hukumu ya maisha ni kinyume na katiba/ Picha: wengine 

Jaji wa Kenya ameamua kuwa hukumu ya maisha ni kinyume na katiba ikiwa haina maelezo yanayoambatana na wakati maalumu.

Hii ni kulingana na jaji Nixon Sifuna aliyekuwa anafanya uamuzi wa kesi inayomhusu baba aliyepatikana na hati ya kumnyanyasa kijinsia mwanaye wa kike wa miaka 10 mwaka wa 2017 katika kaunti ya Muranga nchini Kenya.

Alipewa hukumu Julai 2022 lakini akakata rufaa na na hatimae kufika mbele ya jaji Sifuna.

Ingawa aliamua kuwa kesi dhidi ya mshtakiwa ilikuwa na nguvu, jaji Sifuna alisema hukumu ya maisha ni kama hukumu ya kifo kwa sababu huku siku ya kuanza kwa hukumu inajulikana, tarehe ya kumaliza hukumu ya maisha huwa haijulikani.

"Ni hukumu ya kupotosha kwa sababu ikianza tu mtu hufikiria kuwa siku moja ataimaliza na ataachiliwa kutoka jela," jaji Sifuna alisema.

Jaji huyu aliamua kutoa hukumu ya maisha kwa mshitakiwa na kumpoa miaka 10 gerezani kuanzia 21 Julai 2022 alipohukumiwa.

Mjadala wa hukumu ya kifo na hukumu ya maisha umekuwepo kwa muda huku watetezi wa haki ya binadamu wakizikashifu.

Mwaka 2018 mwanasheri mkuu wa nchi, wakati huo akiwa Githu Muigai aliteuwa kamati ya watu 13 baada ya mahakama ya juu kabisa nchini Kenya na bunge kuanza mikakati ya kufafanua sheria ya hukumu ya kjifo.

Majaji hao wakiongozwa na jaji mkuu wakati huo David Maraga walisema hii inaweza kuhusishwa miaka kadhaa ambayo lazima mfungwa kupitia kabla ya kuzingatiwa kwa masiku kupunguzwa au kupewa msamaha.

TRT Afrika