Jaji mkuu Kenya Martha Koome atoa maelekezo mapoya baada ya hakimu kupigwa risasi / Picha kutoka  Martha Koome

Mahakama Kuu nchini Kenya, imelaani kitendo cha kushambuliwa kwa risasi kwa Hakimu wa Mahakama ya Makadara, iliyopo jijini Nairobi nchini Kenya. Katika taarifa ya vyombo vya habari iliyotolewa na Ofisi ya Mahakama Kuu nchini humo, imeonyesha kusikitishwa kwake na shambulizi hilo lilisababisha kujeruhiwa kwa Hakimu Monica Kivuti.

"Nimejulishwa kuhusu tukio la kushambuliwa kwa risasi katika Mahakama ya Makadara lililohusisha afisa polisi mwandamizi na kumsababishia majeruha Hakimu Monica Kivuti. Mahakama inalaamu tukio hili, na inataka vikosi vya usalama vya taifa kukabiliana na hali hii haraka iwezekanavyo,” Jaji mkuu Martha Koome amesema katika taarifa.

Vurumai hiyo imetokea Juni 13, 2024, ambapo mmoja wa maafisa wa polisi mwandamizi ambae mke wake alifutiwa dhamana baada ya mshtakiwa kukiuka masharti ya dhamana alimpiga risasi hakimu.

Baada ya uamuzi huo kutolewa, ndipo askari huyo alipomfyatulia risasi hakimu na kumjeruhi vibaya mguuni.Hata hivyo, afisa huyo alijibiwa kwa mashambulizi kutoka kwa maafisa wengine waliokuwa katika eneo hilo, na hatimae kukimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

Masharti mapya ya mahakamani

Jaji mkuu ametoa maelekezo mapya kwa ajili ya usalama mahakamani.

" Kitengo cha polisi cha mahakama pamoja na mkuu wa polisi nchini Kenya wameelekezwa kuongeza usalama katika viyuo vyote vya mahakama nchini kote. Pia wameambia kuhakikisha kuwa ni maafisa wa polisi ambao wamesajiliwa na mahakama tu ambao wanaruhusiwa kutoa usalama katiak vituo hivi," Koome amesema.

Jaji mkuu pia ameongezea kuwa mahakama ya Makadara ambapo kisa cha hakimu kupigwa risasi kilitokea itafungwa hado tarehe 17 Juni 2024, na kesi zote ambazo zilifaa kusikizwa katika mahakama hiyo zitasikilizwa kupitia njia ya mitandaoni.

Kamati ya usalama ya mahakama itaangalia tena jinsi ya kuimarisha maswala ya kuboresha usalama katiak kila kituo cha mahakama nchini.

Maafisa wa usalama wa mahakama watapewa mafunzo spesheli.

TRT Afrika